FC Barcelona hoi San Siro dhidi ya AC Milan ,Je Nani kuvuka robo fainali katika Marudiano ya Timu 16 Bora UEFA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 21, 2013

FC Barcelona hoi San Siro dhidi ya AC Milan ,Je Nani kuvuka robo fainali katika Marudiano ya Timu 16 Bora UEFA.

Sulley Muntari

FC  Barcelona wakiwa na Mchezaji Bora Duniani, Lionel Messi, wameonja joto katika mchezo wa soka ndani ya uwanja wa San Siro huko Jijini Milano Italia, baada ya kubondwa Bao 2-0 na wenyeji wao AC Milan katika Mechi ya kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya  UEFA CHAMPIONS LIGI.




Frikiki ya AC Milan ilipenyezwa kwa Riccardo Montolivo alieachia kigongo kilichobabatiza Wachezaji kadhaa na kutua kwa Kevin-Prince Boateng aliefunga Bao la kwanza kwa AC Milan katika Dakika ya 57.



Bao la pili lilifungwa na Sulley Muntari katika Dakika ya 81 baada ya kazi nzuri ya M'Baye Niang na Stephan El Shaarawy.



Huko Uturuki kwenye nyingine , Galasaray, wakiwa na wapya Didier Drogba na Wesley Sneijder, walikamatwa na kutoka sare ya Bao 1-1 na Schalke ya Ujerumani.







RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16   RATIBA.

[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]


MARUDIANO
Jumanne 5 Machi 2013


Borussia Dortmund v Shakhtar Donetsk [2-2]

Man United v Real Madrid [1-1]


Jumatano 6 Machi 2013


Juventus v Celtic [3-0]

Paris St Germain v Valencia [2-1]



Jumanne 12 Machi 2013


Bayern Munich v Arsenal
Barcelona v AC Milan [0-2]

Schalke v Galatasaray [1-1]


Jumatano 13 Machi 2013


Bayern Munich v Arsenal [3-1]

Malaga v FC Porto [1-0]



ROBO FAINALI.


Mechi ya 1=Tarehe 2 na 3 Aprili 2013

Mechi ya 2= Tarehe 9 na 10 Aprili 2013


NUSU FAINALI.


Mechi ya 1= Tarehe 23 na 24 Aprili 2013

Mechi ya 2= Tarehe 30 Aprili  na 1 Mei 2013



FAINALI


25 Mei 2013


UWANJA wa WEMBLEY, London.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad