Tazama picha za ofisi yake mpya 'Endless Fame Film' iliyoitambulisha rasmi na inatarajia kuanza kazi mwezi wa tatu mwaka huu.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 21, 2013

Tazama picha za ofisi yake mpya 'Endless Fame Film' iliyoitambulisha rasmi na inatarajia kuanza kazi mwezi wa tatu mwaka huu..

Wema Abrahamu Sepetu
Msanii wa tasnia ya filamu Bongo, Wema Abrahamu Sepetu kutangaza kuwa anamiliki kampuni mpya ya filamu"Endless Fame Film" leo mchana aliweza kufanya press conference na waandishi mbalimbali huku akitambulisha rasmi kampuni hiyo.


 

Wema anasema  Kwa mujibu wa msanii huyu alisema kwamba kwa  sasa bado ofisi yake haijaanza kufanya kazi ila inatarajia rasmi kuanza kazi mwezi wa tatu mwaka huu.



    Tazama picha za ofisi yake mpya 'Endless Fame Film' iliyoitambulisha leo rasmi.......



Japokua mwigizaji Wema Sepetu hakua tayari kutaja kiasi cha pesa kilichogharimu ofisi yake mpya aliyoifungua, amekubali kwamba ilimchukua miezi 6 toka ameanza kuishughulikia, ni ofisi ambayo itahusika kwa kiasi kikubwa kuandaa movie zake pamoja na movie za waigizaji wengine.


Mpaka sasa ameshatoa ajira kwa vijana wenzake sita na bado anasema kuna nafasi za ajira kwa vijana ambao wanadhani wanavigezo vya kufanya kazi ya utengenezaji movie wakiwa ni wataalamu wa vitu mbalimbali.


Kampuni hiyo itakua pia inahusika na kuvifanyia kazi vipaji vya waigizaji wapya na kuwapa nafasi ya kuonekana wakiwa tayari na mikataba mizuri chini ya usimamizi wa Wema Sepetu likiwa pia ni moja ya malengo yake kwenye hiyo kampuni.


Mama mzazi wa Wema anasema anamshukuru sana Marehemu Kanumba manake ndio alimshawishi ampe Wema ruhusa ya kuingia kwenye uigizaji mpaka kutimiza ndoto kama hii.

    Wema na Dotnata

Mama mzazi wa Wema katika ofisi ya Wema ambayo ipo ghorofa ya kwanza kwenye nyumba ambayo ipo Kinondoni Dar es salaam karibu na Biashara Complex.

Wema na Zamaradi

Wema na Rich

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad