Cheki Picha kali za Mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa kati ya Ngara Starz (Ngara Tanzania) v/s Lion FC ya (Buhinda Burundi) mchezo ukikichezwa uwanja wa Kobero -Burundi na Ngara Starz kuchapwa bao 2-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, February 22, 2013

Cheki Picha kali za Mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa kati ya Ngara Starz (Ngara Tanzania) v/s Lion FC ya (Buhinda Burundi) mchezo ukikichezwa uwanja wa Kobero -Burundi na Ngara Starz kuchapwa bao 2-0.



Mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa kati ya Ngara Starz (Ngara Tanzania) v/s Lion FC ya (Buhinda Burundi) mchezo ukikichezwa uwanja wa Kobero -Burundi na Ngara Starz kuchapwa bao 2-0 ugenini na Nyumbani.


Kikosi cha wachezaji 11 wa Ngara Starz (wilayani Ngara mkoani kagera Tanzania wakiwa na Kocha wao Mwl.Said Salumu mwenye track suit nyeusi.

Hiki ndicho Kikosi cha wachezaji 11 wa Lion FC ya Buhinda –Burundi wakiwafunga Ngara Starz  bao 2-0.

 Kikosi cha  Lion FC ya Buhinda –Burundi wakifanya mazoezi mepesi kabla ya kuanza mchezo huo katika uwanja wa Kobero-Burundi.

Kikosi cha  Ngara Starz  katika Mazoezi Mepesi kabla ya Mchezo.

Hawa ndio marefali waliochezesha mchezo huo kati ya  Lion FC ya Buhinda –Burundi wakiwafunga Ngara Starz  bao 2-0.

(Mwenyesuti ya Kaki)Alex Gashaz mwenyekiti wa chama cha soka wilayani Ngara NDFA akiteta jambo na mchezaji wa Ngara Starz huku pembeni (Mohamed R.Makonda mwandishi na Mtangazaji wa Radio Kwizera FM-Ngara,Mrisho Salum Tozo na Mdau wa Michezo toka Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mkoani Kagera -Tanzania.


Mkuu wa wilaya ya Buhinda akisalimiana na  wachezaji wa Ngara Starz.

Diwani wa Kata ya Ngara Mjini CCM-Chalz Kwizera Rujuba akisalimiana na Wachezaji huku mwenye Jezi nyekundu ni Diwani wa Viti maalumu CCM-Tarafa ya Kanazi.

Afisa Elimu wilaya ya Ngara -Saimon Mumbee nae alikuwepo na ni mmoja ya mdau mkubwa wa Michezo.

Benchi la wachezaji wa Ngara Starz  .
Benchi la wachezaji wa Lion FC  .
Afisa Utumishi Wilaya ya Ngara (mwenye flana ya kaki)akifatilia mchezo huo katika uwanja wa Kobero-Burundi ambapo Ngara Starz walifungwa bao 2-0 na Lion FC..
Mwenye suti nyeusi ni Mwenyekiti wa chama tawala nchini Burundi cha CNDD FDD mkoa wa Muyinga.
Mashabiki mbalimbali wakifatilia mchezo huo uwanjani kobero.
Baada ya kuwashinda bao 2-0 Ngara Starz-Lion FC wakakabidhiwa Kikombe na Mkuu wa Mkoa wa Muyinga nchini Burundi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad