Sare kama kwaida AFCON 2013 - Nigeria 1 Zambia 1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 25, 2013

Sare kama kwaida AFCON 2013 - Nigeria 1 Zambia 1.

Zambia
Mchezo  kati ya miamba wawili wa soka barani Afrika  Nigeria na Zambia  umemalizika huku  timu hizo zikitoka sare ya kufungana bao  1 - 1.


 

Mechi hiyo ambayo ilitabiriwa  kuwa moja ya mechi ngumu zaidi katika hatua ya makundi ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika inayoendelea nchini  Afrika Kusini lakini  ilianza kwa mashambukizi katika pande zote na kunako dakika ya 25,mlinda lango wa Zambia Davies Nkausu alimfanyia madhambi mshambulizi wa Nigeria Ahmed Musa na hivyo refa wa mechi hiyo kutoa penalti kwa Nigeria.



Lakini mcheza kiungo wake John Obi Mikel  ambaye pia anaichezea klabu ya Chelsea akapoteza penalti hiyo na hivyo kuwapa Mabingwa hao watetezi nafasi nyingine ya kupumua.



Katika kipindi hicho cha kwanza timu hizo mbili zilionekana kutoshana nguvu huku pande zote zikifanya mashambulio ya mara kwa mara.



Nigeria ilianza kipindi cha pili kwa kasi zaidi na kufanya mashambulio kadhaa katika lango la Chipolopolo.



Na baada ya kupoteza mkwaju wa penalti John Obi Mikel, alijiimarisha zaidi kipindi cha pili na kunako dakika ya 56 Nigeria ikapata bao lake la kwanza kupitia kwa mshambulizi wake matata Emmanuel Emenike.



Kunako dakika ya 84 mlinda lango wa Nigeria alimuangusha mshambuliaji wa Zambia Emmanuel Mayuko, na refa wa mechi hiyo sawa na alivyokuwa amefanya katika kipindi cha kwanza akaipa Zambia penalti ambayo iliwekwa kimyani na kipa za Chipolopolo Kennedy Mweene.



Nigeria sasa ina alama mbili sawa na Nigeria na itabidi washinde mechi zao za mwisho siku ya jumapili ili kufuzuz kwa hatua ra robo fainal.



Awali Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, amewaandikia wachezaji wa Super Eagles na kuwapa ushauri wa jinsi ya kucheza mechi hiyo.



Kocha wa Nigeria, Stephen Keshi, vile vile alifika mbele ya viongozi wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria, kuelezea kwa nini hawakushinda mechi yao ya ufunguzi.



Mechi ya pili katika kundi hilo kati ya Ethiopia na Burkina Faso kuanza mwendo wa saa tatu za usiku majira ya Afrika mashariki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad