Mamia wajitokeza katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kumpumzisha mpendwa wao, Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, January 04, 2013

Mamia wajitokeza katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kumpumzisha mpendwa wao, Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki'



MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam leo wamejitokeza katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kumpumzisha mpendwa wao, Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki', aliyefariki dunia alfajiri ya Januari 2, mwaka huu (Jumatano) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


 Miongoni mwa waliomzika Sajuki ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.


(PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)

Waombolezaji wa Msiba wa Msanii wa Filamu hapa nchini,Marehemu  Sadick Juma Kilowoko wakibeba jeneza lenye mwili wake tayari kwa taratibu za kwenda Mazikoni,wakitokea Nyumbani kwa Marehemu Tabata Bima.


Mwili umezikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.


Pamoja na kwamba kulikuwa na Mvua kubwa lakini hakuna alitaka kuondoka msibani hapo mpaka pale mwili ulipoondoka kuelekea Msikitini kwa Kusalia na baadae kwenye Mazishi.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki'.


Baba mzazi wa Sajuki, Mzee Kilowoko, akiweka udongo katika kaburi la mwanaye.


Makabulini Kisutu Dar.


Umati wa watu uliojitokeza hapa katika makaburi ya kisutu upanga kumpumzisha mpendwa wetu Sajuki.




Marehemu Sajuki’’alilazwa katika hospitali ya Muhimbili   kwa wiki mbili ambapo alikua anasubiri kupata urahisi wa kusafiri kurudi India kwenye matibabu ambayo alipangiwa kurudi tena December 2012.

 

Mwezi wa tano mwaka jana watanzania tulichanga kadri ya uwezo wetu ili akatibiwe India.Ni kweli alienda India kwenye matibabu na alifanyiwa upasuaji.Ila matibabu yake yalikuwa yakiendelea ambapo ilikuwa lazima arudi tena India mwezi uliopita 2012.



  Baada ya kurudi nchini hali yake ilikuwa nzuri tu na mwili ukaanza kurejea kama anavyoonekana kwenye picha hapo akiwa na Wastara mkewe.Pamoja na kuwa katika hali hii bado alikuwa ni mgojwa.





Mwezi wa kumi na moja 2012 Sajuki alifanya tour aliyoiita asante Tanzania kwa lengo la kuwashukuru watanzania walipomchangia.



Lakini kilichokuwa nyuma ya pazia ni kwamba alikuwa akikusanya pesa ili arudi India kwa matibabu.



Akiwa mkoani Arusha  katika  Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini  hivi karibuni alianguka.Na yeye mwenyewe kukiri kwa kusema “Sijisikii vizuri, hali yangu ni mbaya.”


Baadae mwenyewe alisema kuwa pamoja na kuumwa,haikuwa rahisi kurudi katika vyombo vya habari tena kwa ajili ya kuomba Watanzania kumchangia kwa ajili ya fedha za matibabu kwa awamu nyingine. na muda wa kurudi ulikuwa umefika.




Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania,

Mh. Jakaya Mrisho Kikwete

akiweka udongo kwenye

Kaburi la Marehemu

Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI)

wakati wa Mazishi yake

yaliyofanyika mchana huu

kwenye Makaburi ya Kisutu,

Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na msaada lakini bado kulikuwa na changamoto kwamba tatizo kubwa lililomzuia Sajuki kurudi India ni pumzi ambapo walikua wanatafuta ndege yenye huduma ya gesi.



Baada ya kuhangaika sana, dakika za mwisho ndio walikua wamepata ndege ambayo imekubali kutoa huduma ya gesi kwa Sajuki ambapo Shirika la ndege la Emirates ndio lilikua limekubali kutoa huduma hiyo kumsafirisha mpaka India.



Sajuki alikua na tatizo kubwa la kupumua wakati huu ambapo   upumuaji wake ulikua unabadilika mara kwa mara.



 Pole sana Wastara ulijitahidi kadri ya uwezo wako kuhakikisha mumeo anapona.



Ila yule aliyetuumba ndio ameamua na akipanga lake hakuwa wa kulipangua.Pole kwa familia,mashabiki na watanzania kwa ujumla.



Kwa mujibu wa baba yake mzazi,marehemu alizaliwa mwaka 1986 na amefariki akiwa na umri wa miaka 27.



…. Mungu ailaze roho ya marehemu Juma Kilowoko (Sajuki) mahala pema peponi, Amen.

2 comments:

  1. Inalillah waina_ilaih raahiun

    ReplyDelete
  2. pumzika salama Sajuki, nilikupenda na kukubali na ntaendelea hivyo daima. R.I. P

    ReplyDelete

Post Bottom Ad