Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi klabu bingwa ya Tanzania bara timu ya Simba SC yaanza vizuri mbio za kuutetea ubingwa wake wa Mapinduzi kwa kuichapa Jamhuri ya Zanzibar kwa mabao 4-2. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 03, 2013

Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi klabu bingwa ya Tanzania bara timu ya Simba SC yaanza vizuri mbio za kuutetea ubingwa wake wa Mapinduzi kwa kuichapa Jamhuri ya Zanzibar kwa mabao 4-2.


Haruna Chanongo aliyeruka

 kufunga bao la kwanza la Simba SC
Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi klabu bingwa ya Tanzania bara timu ya Simba SC ya Dar leo imeanza vizuri mbio za kuutetea ubingwa wake wa Mapinduzi kwa kuichapa Jamhuri ya Zanzibar kwa mabao 4-2 katika mchezo uliochezwa  huko visiwani Zanzibar.


 

Katika mchezo huo mabao ya Simba yalifungwa na kinda Haruna Athumani Chanongo aliyepiga mawili, Felix Sunzu na Shomari Kapombe wakitupia kambani goli moja kila mmoja.



Jamhuri ndio walikuwa wa kwanza kuliona goli la Simba katika robo ya kwanza ya mchezo kwa goli lilofungwa na Mfanyeje Mussa, kabla ya Simba kusawazisha katika dakika ya 27, na baadae kidogo akaongeza bao la pili kwa shuti kali,Mfanyeje tena aliwaumiza tena Simba na timu zikaenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu.



Awamu ya pili ya mchezo Simba walirudi vizuri na kupata mabao mawili yaliyofungwa na Felix Sunzu na Shomari Kapombe na kuipa timu yao ushindi wa kwanza ndani ya mwaka 2013. 



Aman Ibrahim Makungu.
Kabla ya mchezo huo, Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad alizindua mashindano hayo kwa kupiga penalti na kumfunga kipa wa Jamhuri, Jaffar.



 Akiongozwa na raisi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Aman Ibrahim Makungu, Mh Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, alizikagua timu zote mbili kabla ya kuanza kucheza.




Liewig kushoto akisaini mkataba wa

miezi 18 kuifundisha Simba.

 Kulia Makamu Mwenyekiti

wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu'
Kocha mpya wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig alikuwa jukwaani akiishuhudia timu, ikiongozwa na watakaokuwa wasaidizi wake, Mganda Moses Basena na mzalendo, Jamhuri Kihwelo.



Katika mchezo uliotangulia, Tusker ya Kenya iliichapa Bandari ya hapa mabao 5-1, mabao ya Jesse Were 29 na 43, Ismail Dunga 35 Michael Olunga dakika ya 89 na Andrew Tolowa dakika ya 90, wakati la Bandari lilifungwa na Amour Janja dakika ya 83. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad