![]() |
IGP Said Mwema.
|
Mkuu wa
wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu amewataja waliouawa katika tukio hilo
kuwa ni Sajent Thomas na Koplo Damas wote wa kituo cha Polisi Kasulo wilayani
Ngara.
Bw Kanyasu amesema
kuwa tukio hilo limetokea Januari 6 mwaka huu kati ya saa moja hadi saa nne
usiku ambapo Askari hao wameuawa na wananchi baada ya kuanza kurusha risasi
hewani waliposimamishwa na wananchi baada ya kuwekewa vizuizi barabarani
wakidhaniwa kuwa majambazi.
Aidha amesema
kuwa Askari hao ambao walikuwa wakitumia gari binafsi la askari mmoja wao
wakiwa wamevaa kiraia ,baada ya kufika eneo hilo walishambuliwa na wananchi
hadi kupoteza maisha na kwamba Askari aliyekuwa na silaha alifanikiwa kukimbia.
Bw Kanyasu
amesema kuwa askari hao wa kituo cha Kasulo wilayani Ngara walikuwa na
mtuhumiwa waliyemkamata akiwa na meno ya tembo lakini hawakutoa taarifa kwa
uongozi wa wilaya ya Karagwe licha ya kupita katika vizuizi vya pori la Burigi
mkoani Kagera.
![]() |
Karagwe |
Miili ya Askari
Polisi hao waliouwawa imehifadhiwa katika hospitali ya Nyakahanga
wilayani Karagwe.
Katika tukio
hilo kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Juvenari Joseph amepigwa risasi
kwenye kiganja na kulazwa katika hospitali ya Kayanga.
Kamanda wa
polisi mkoani Kagera Bw Philip Kalangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo chake.
Duh nyumbani Huko, Poleni wafiwa Na Asante kwa manewz ya ukweli Makonda
ReplyDelete