Cheki Uzembe wa Madereva unavyosababisha ongezeko Kubwa la Ajali za Barabarani hapa Nchini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, November 14, 2012

Cheki Uzembe wa Madereva unavyosababisha ongezeko Kubwa la Ajali za Barabarani hapa Nchini.


Pamoja na Alama ya Kona kwenye mteremko mkali, dereva wa Bus Sumry anaonekana kukaidi na kuamua kulipita Bus jingine jambo ambalo ni hatari kwani linaweza kusababisha ajali mbaya endapo litatokea gari jingine mbele.


Ajali nyingi za barabarani nchini husababishwa na madereva wazembe wasio zingatia sheria za matumizi sahihi ya barabara. Miongoni mwa ajali hizo nyingi husababishwa na madereva hao kuovatake magari mengine katika kona au milima kama basi hili linavyofanya katika kona ya Lugalo mkoani Iringa. Madereva “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.


Basi la Taqwa likiwa limehariba katika mlima Kitonga .


Basi hili lingine nalo lilikuwa linafanya makosa hayo hayo ya kulipita gari lingine katika mwiinuko na kona kali ya mlima Kitonga.


Lori la mizigo lililosheheni mbao likiteremka mlima Kitonga  ambapo Askari wa Usalama barabarani  nchini wametakiwa kuongeza doria katika mlima huo kufuatia ajali za mara kwa mara zinazotokea kutoka na madereva kuendesha kwa fujo bila kuzingatia usalama barabarani.


Mteremko wa Mlima Kitonga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad