Waziri Sitta aipongeza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa kukabiliana na vitendo vya uharifu huku ziara yake ikikubwa na ajali ya gari la Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 30, 2012

Waziri Sitta aipongeza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa kukabiliana na vitendo vya uharifu huku ziara yake ikikubwa na ajali ya gari la Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda.


 Hapo jana  tarehe 29/08/2012 Katika  ziara Mheshimiwa Samwel Sitta Wazira wa Jumuiya ya Afrika Mashari Kutoka Wilaya ya Karagwe kuelekea Wilaya ya Kyerwa kulitokea ajali ya garia la Ofisa wa Ubalozi  wa Tanzania Nchini Uganda aliyekuja kuungana na Mhe. Sitta katika ukaguzi wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Aidha akiwa wilayani Ngara mkoani Kagera Waziri wa Africa Mashariki Bw.Samweli Sitta amesema kitendo cha mipaka baina ya Tanzania na nchi , kufanya kazi kwa saa 12 kinadumaza maendeleo katika jumuiya  hiyo ya EAC.


Waziri Sitta amesema hayo leo wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalaama ya wilaya ya Ngara katika ofisi ya mkuu wa wilaya na kwamba mipaka hiyo inapaswa kufanya kazi kwa saa 24 ili kurahisisha biashara katika nchi hizo.


Ajali hiyo ilitokea muda wa saa 5:15 asubuhi katika eneo la Lukole katika Kata ya Ihanda baada ya kuyumba na kuacha njia na kuangukia upande mmoja. Katika ajali hiyo hakuna mtu yeyote aliyeumia wote Ofisa wa Ubalozi na Dereva wake walitoka salama jambo ambalo halikuidhuru ziara ya Mhe. Sitta na kuendelea mpaka Wilayani Kyerwa Murongo.

 Katika hatua nyingine Bw Sitta ameipongeza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa kukabiliana na vitendo vya uharifu ikiwemo ujambazi wa kutumia silaha.

 
Na:Mwana wa Makonda  na  Bukoba wadau.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad