Wananchi wa kata ya Murusagamba wilayani Ngara mkoani Kagera wametaka katiba itakayoundwa iweke sharia ya kuwabana wasichana wanaobeba ujauzito . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 07, 2012

Wananchi wa kata ya Murusagamba wilayani Ngara mkoani Kagera wametaka katiba itakayoundwa iweke sharia ya kuwabana wasichana wanaobeba ujauzito .


Katika mchakato wa kutoa maoni ya kuundwa kwa katiba mpya unaendelea Mkoani Kagera,Wananchi wa kata ya Murusagamba wilayani Ngara  mkoani Kagera wametaka katiba itakayoundwa iweke sharia ya kuwabana wasichana wanaobeba ujauzito wakiwa shuleni badara ya kuwabana wavulana peke yake.

Akitoa maoni kwa tume ya kukusanya maoni ilianza leo mmoja wa wananchi wa kiji cha Murusagambga Bi. Pendo Alfonce amesema katiba iliyopo haijaaninisha hatua zipi zinachukuliwa kwa wasichana wanaobeba ujauzito wakiwa shuleni na badara yake imekuwa ikiwabana wavulana .

Amesema katika uundwaji wa katiba hiyo pia iweke wazi mavazi yanayositahili kuvaliwa na wanawake hususani wasichana, wanavaa nguo zinazodhalilisha tamaduni za kitanzania.

Zoezi la kukusanya maoni ya kuundwa kwa  katiba mpya limeanza wilayani Ngara july 6 mwaka huu  na linataraji kukamilika jumapili july 8 mwaka huu kwa kukusanya maoni ya wakazi wa kata ya Ngara mjini pamoja na Rusumo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad