Mtoto mwenye umri wa wiki tatu amekufa kutokana na kunyongwa na baba yake mzazi wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 10, 2012

Mtoto mwenye umri wa wiki tatu amekufa kutokana na kunyongwa na baba yake mzazi wilayani Ngara mkoani Kagera.


Magari yaJeshi la polisi  mkoani Kagera.

Mtoto mwenye umri wa wiki tatu katika eneo la Nakatunga wilayani Ngara mkoani Kagera amekufa kutokana na kiachoelezwa kuwa ni kunyongwa na baba yake mzazi aliyetabuliwa kw a jina la Adam Ibrahim.

Mama mzazi wa mtoto huyo  Bi Ombeni   Paschal amesema tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Nakatunga mjini Ngara.

Bi  Paschal amesema mtoto huyo   alipiga kelele wakati akiwa amepakatwa na baba yake ambaye alimrejesha kwa mama yake akiwa anatoka   povu  mdomoni   kabla ya kufariki .

Mganga   mfawidhi  wa hospitali  ya Nyamiaga  wilayani Ngara  Dr  Rafael   Rwezaura  amesema  wamepeleka sampuli  kwa mkemia mkuu wa serikali ili kubaini chanzo cha kifo hicho.

Jeshi la polisi wilayani Ngara limethibitisha  kutokea kwa tukio hilo  na kwamba linamtafuta mtuhumiwa ambaye ametoroka.



Tembo wanazidi kuuwawa barani Afrika kutokana na kuongezeka kwa biashara ya pembe nchini China

Katika hatua nyingine, Mkazi wa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera aliyekuwa akichunga ng’ombe amefariki baada ya kukanyagwa na Tembo .

Afisa tarafa ya Nyamiaga  Bw  Godian  Bagombweki   amemtaja  aliyefariki kuwa ni Jofrey  Kamanzi Kalekezi mwenye umri wa miaka 24 na  kwamba tukio hilo limetokea ijumaa ya wiki iliyopita.

Amesema tukio hilo limetokea wakati vijana watano waliokuwa wakichunga ng’ombe kukutana ghafla na kundi la tembo ambao walianza kuwakimbiza ndipo mmoja wao akakanyagwa na tembo huyo.

Bw Bagombweki amesema kitendo cha tembo kuwadhuru binadamu kinasababishwa na majangili wanaoingia ndani ya hifadhi na kuwauwa, na baadhi ya wafugaji kulisha mifugo ndani ya hifadhi hali inayosababisha tembo kutoroka na kuingia katika maeneo ya makazi ya watu .


Source ' RK FM

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad