Jumla ya risasi 222 na magazine mbili zimeokotwa katika kijiji cha Mgombe wilayani Kasulu huku wahamiaji haramu 196 wakikamatwa wilayani Kibondo mkoani Kigoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, July 07, 2012

Jumla ya risasi 222 na magazine mbili zimeokotwa katika kijiji cha Mgombe wilayani Kasulu huku wahamiaji haramu 196 wakikamatwa wilayani Kibondo mkoani Kigoma.


Jumla ya risasi 222 na magazine mbili zimeokotwa katika kijiji cha Mgombe wilayani Kasulu mkoani Kigoma  baada ya kudondoshwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi.

Jeshi la polisi wilayani Kasulu  limesema kuwa mwenyekiti wa kijiji  hicho Bw. Daud Paul akiwa doria na askari mgambo waliwakimbiza watu wasiofahamika na kudondosha kifurushi kilichookotwa na mwenyekiti huyo pamoja na mgambo hao.

Amesema katika upekuzi huo walikuta kitako cha bunduki, risasi 222 za SMG na SR ambapo kati ya hizo 60 zilikutwa kwenye magazine mbili .

Taarifa kutoka jeshi la polisi wilayani Kasulu zimesema kuwa tukio hilo limetokea July 2 na kwamba hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.

Wakati huo huo, Idara ya uhamiaji katika halmashauri ya wilaya ya Kibondo imewakamata wahamiaji haramu 196, katika zoezi la kuwasaka raia wa kigeni wanaoingia na kuishi nchini kinyume na sharia.

Kaimu afisa uhamiaji wa wilani Kibondo Bw.Fredrick Adam amesema  katika hatua ya awali ya utambuzi wa uraia, tayari wahamiaji haramu 111 wamefukuzwa nchini na wengine 26 wanaendelea kufanyiwa uchunguzi ili kuweza kubaini asili yao na uraia.

Aidha ametoa wito kwa jamii kushirikiana na idara ya uhamiaji ili kuwabaini wahamiaji haramu wano ingia na kuishi nchini kinyume na sharia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad