Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal Mstaafu Fabian Massawe, amezitaka halmashauri za wilaya Mkoani Kagera, kuwasimamia mawakala wa kukusanya mapato ili yapatikane kwa wakati. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 13, 2012

Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal Mstaafu Fabian Massawe, amezitaka halmashauri za wilaya Mkoani Kagera, kuwasimamia mawakala wa kukusanya mapato ili yapatikane kwa wakati.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe Akiongea na Waheshimiwa Madiwani na Wataalam wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Wakati wa Kikao cha Kujadili Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Katika Ukumbi wa Manispaa ya Bukoba.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal Mstaafu Fabian Massawe, amezitaka halmashauri za wilaya Mkoani humo, KUWASIMAMIA mawakala wa kukusanya mapato ili YAPATIKANE kwa wakati.

Kanal Massawe ametoa wito huo, kupitia hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyasu, katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi mjini Ngara.

Amesema kuwa kitendo cha mawakala wa ukusanyaji wa mapato, KUTOWASILISHA mapato kwa wakati katika Halmashauri, kinarudisha nyuma maendeleo ya Halmashauri husika na mkoa kwa ujumla.

Aidha amezishauri Halmashauri za wilaya mkoani humo, kuwa na utaratibu wa kuingia mikataba ya muda mfupi na mawakala hao, ili kurahisisha kuratibu mwenendo wa uwasilishaji wa mapato, unaofanywa na mawakala husika.

 


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe Akiongea na Balozi wa Uingereza Bi Diane Corner na Ujumbe Wake Mara Baada ya Kuwasili Mkoani Kagera na Kufika Ofisini Kwake Kumsalimia.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Massawe katika kikao hicho alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba na Halmashauri zote za mkoa wa Kagera kuhakikisha zinafanya vizuri zaidi katika baadhi ya miradi mfano TASAFU, barabara na sekta ya maji.

Kanal  Massawe aliwakemea wakaguzi wa ndani kuhusu kutotoa taarifa za ukaguzi ubadhilifu wa fedha na wakati wapo katika halmashauri na hoja kuibuliwa na wakaguzi toka nje. Vilevile aliagiza kila baada ya miezi mitatu wakaguzi wa ndani wa Halmashauri zote kuwasilisha taarifa zao katika ofisi yake.

Aidha Halmashauri zote zimeagizwa kutunza nyaraka mbalimbali kwa ajili ya ukaguzi, kuchukua hatua dhidi ya watendaji wazembe, kusimamia ulipwaji wa mishahara ya watumishi pia na kuimarisha kamati za ukaguzi zilizoundwa kisheria na kukusanya kodi kwa kiwango cha kuridhisha.

Mwisho Mkuu wa Mkoa alisistiza kuwa hatosita kuchukua hatua za kinidhamu kwa mtendaji au Halmashauri yoyote itakayofanya kazi zake kwa uzembe bila kuzingatia kanuni sheria na taratibu zilizopo.

Pia alisema hataki kusikia tena katika mkoa wa kagera kuna Halmashauri yenye hoja za ukaguzi kuanzia mwaka huu wa fedha 2011/2012.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad