SIMBA YATWAA KOMBE LA URAFIKI UWANJA WA TAIFA KWA MATUTA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, July 13, 2012

SIMBA YATWAA KOMBE LA URAFIKI UWANJA WA TAIFA KWA MATUTA.

Waziri asiye na Wizara maalum Zanzibar Mh. Machano Othman Said akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya Urafiki nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma mara baada ya timu ya Simba kuifunga timu ya Azam FC magoli 5-3 kwa penati,  baada ya kutoka suluhu magoli 2-2 katika kipindi cha dakika tisini, kwenye mchezo mzuri na wa kuvutia kwa timu zote uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo hivyo kuifanya Simba kuibuka mabingwa wa kombe hilo.

Kwenye Fainali iliyochezwa leo Uwanja wa Taifa Dar es Salaam baada ya kuhamishwa kutoka Zanzibar, Simba ilifanikiwa kutwaa Kombe baada ya kuitoa Azam FC kwa Mikwaju ya Penati 4-3 kufuatia sare ya bao 2-2 katika Dakika 90.

Mchezaji wa kimataifa wa timu ya Simba kutoka nchini Zambia Felix Sunzu akichuana vikali na beki wa timu ya Azam FC katika mchezo huo.

Simba ndio walitangulia kufunga bao la kwanza kupitia Felix Sunzu na Azam wakasawazisha kwa bao la Mcha katika Dakika ya 45.

Kipindi cha Pili Azam wakafunga Bao la Pili kupitia John Bocco na Simba kurudisha kwa Penati ya Mwinyi Kazimoto.


Wachezaji wa timu ya Simba pamoja na kocha wao wakipiga picha pamoja na kombe lao walilolikabidhiwa leo kwenye uwanja wa Taifa baada ya kuifunga timu ya Azam FC katika michuano ya Urafiki inayoandaliwa visiwani Zanzibar.

Ubao wa matangazo ukionyesha Simba 5 Azam FC 3 kwenye uwanja wa Taifa.

Ndipo ikaja bahati nasibu ya Penati na Simba kushinda kwa Bao 4-3.

Wachezaji wa timu ya Simba wakimnyanyua juu juu golikipa wao Juma K. Juma baada ya kupangua penati mbili katika mchezo huo uliokuwa wa fainali katika michuano ya Urafiki.

Kwa ushindi huu, Simba wamenyakua Zawadi ya Shilingi Milioni 10 na Azam kupewa Milioni 5.


Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia mara baada ya kuifunga timu ya Azam FC kwenye uwanja wa Taifa.

Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia timu yao.

Mashabiki wa timu ya Azam FC wakishangilia timu yao.

 Kikosi cha Azama kilichoanza.

Kikosi cha Simba kilichoanza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad