Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA),akiwa na Wasani wa kundi la Kigoma Allstarz. |
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA),
amesema Kampuni ya mtandao ya Onmobile inashirikiana na makamupni ya simu za
mikononi kuwanyonya wasanii kwa kuwalipa asilimia ndogo ya mapato yanayotokana
na matumizi ya nyimbo zao.
Akichangia
hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia iliyosomwa
bungeni mjini Dodoma jana, Zitto alisema kinachoshangaza kampuni hiyo
iliyohodhi mambo yote ya kampuni za Vodacom na Airtel, inafanya kazi bila
leseni.
“Ukimpigia
simu Waziri Mkuu… utasikia simu yake ina wimbo wa Rose Mhando, Naibu Waziri
Adam Malima yeye upo wimbo wa Dar mpaka Moro wa Wanaume Familly na ukinipigia
mimi utasikia Kurani ama wimbo wa CHADEMA.
“Lakini
kinachoshangaza wasanii hawa wananyonywa licha ya nyimbo zao kutumika,
tunadhani wasanii wanapata… si kweli kwani hata vituo vya redio na televisheni
vya serikali vinatumia nyimbo hizi bila kuwalipa chochote.
Zitto
alipendekeza kuwa, wakala huyo afukuzwe nchini kwa kuisababishia nchi hasara na
kushauri kipato cha wasanii kupitia nyimbo zinazotumika kwenye miito ya simu
kiongezwe hadi asilimia 50 ili kuwawezesha kujikimu kimaisha.
“Wasanii
wapate haki yao na walipwe kutokana na jasho lao. Kazi ya dola ni kumlinda
mnyonge. Kampuni za simu ni giant (kubwa), ukiwauliza wanasema hawana mkataba
na wasanii. Kwa nini kampuni hiyo ifanye kazi bila leseni?” alihoji.
Imani ni nguvu inayoishi, ‘’imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana>> hivyo >> MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI (HABAKUKI 2:4) |
Nyimbo hizo
ni zile ambazo mteja wa mtandao husika, huomba ili akipigiwa simu asikie wimbo
huo na huduma hiyo hutozwa Sh300 kwa kila wimbo.
Uchunguzi
ulibaini kuwa, kila siku Kampuni ya Airtel hupata Sh15 milioni huku Vodacom
wakipata karibu Sh20 milioni kutokana na bishara hiyo.
Makampuni
makubwa ya Vodacom na Airtel wameingia mkataba na Onmobile na wanaingiza sh
bilioni 43 kutokana na milio,” alisema mbunge huyo aliyeonyesha nia ya kuutaka
urais mwaka 2015 kupitia chama chake.
Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alilieleza gazeti hili kuwa, alikuwa hafahamu
kwamba Kampuni ya Onmobile ilikuwa ikifanya kazi nchini, kwani awali waliipa
masharti ambayo ilipaswa kuyatimiza kabla ya kupewa leseni.
Aliyataja
masharti hayo kuwa ni pamoja na kueleza zilipo ofisi zao nchini kutaja wanahisa
wao; shughuli wanayotaka kuifanya pamoja na mambo mengine.
Kuhusu
ushiriki wa Vodacom na Airtel katika biashara hiyo Profesa Nkoma alisema: “Sina
taarifa kama wanafanya kazi. Unachotakiwa kufanya, zungumza na Airtel na
Vodacom wakueleze kwa nini wanafanya kazi na kampuni ambayo haina leseni.”
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba |
Naibu Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba akijibu hoja za wabunge
jana jioni alisema kuwa, tayari Serikali imeizuia Kampuni ya Onmobile kutoa
huduma kutokana na kutokuwa na usajili kisheria.
“Kampuni hii
iliomba kibali cha kufanya kazi hii Februari 29, mwaka huu pale TCRA, lakini
ukweli ni kuwa, ilinyimwa kwa sababu haikuwa na usajili wa Brela,” alisema
Makamba.
Kuhusu wizi
wa kazi za wasanii, naibu waziri huyo alisema umekuwa ukifanywa pia kwa njia
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutopata mrabaha nyimbo zao zinapochezwa redioni
na kwenye televisheni.
No comments:
Post a Comment