Kikosi cha Azam FC |
Timu za Tanzania, Mabingwa watetezi Yanga na Azam FC , leo zimeshinda Mechi zao za Nusu Fainali za mashindano ya kombe la Kagame , Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, na kutinga Fainali ambayo inahakikisha Kombe hilo litabaki Tanzania.
Katika Nusu Fainali ya kwanza, bao la Dakika ya 89 la Supastraika Mrisho Ngassa liliwapa Azam FC ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Vita Club ya Congo DRC katika Mechi ambayo Azam FC walitanguliwa kufungwa katika Dakika ya 34.
Kipindi cha pili pasi ya Tchetche iliunganishwa vyema na Bocco aliefunga bao la kusawazisha katika Dakika ya 68 na Mchezaji alietoka benchi, Mrisho Ngassa, alimalizia pasi murua ya Salum Abukar na kupiga bao la ushindi.
Kwenye Nusu Fainali iliyofuatia, ngoma ilikuwa ngumu mno kati ya Yanga na APR ya Rwanda na hadi Dakika 90 bao zilikuwa 0-0 na zikaongezwa Dakika 30 za nyongeza.
Yanga walipata bao lao moja na la ushindi katika Dakika ya 100 baada ya krosi ya Niyonzima kuunganishwa kwa kifua na Hamisi Kiiza 'Diego'.
Kiungo Haruna Niyonzima wa Yanga. Zamani alikuwa mchezaji wa APR |
Dakika 3 baadae Yanga walipata pigo pale Mchezaji wao Godfrey Taita kuwashwa Kadi Nyekundu na hivyo hatacheza Mechi ya Fainali hapo Jumamosi.
MSHINDI WA 3:
Julai 28 Jumamosi
[Saa 8 Mchana]
Vita v APR
FAINALI:
Julai 28 Jumamosi
[Saa 10 Mchana]
Azam v Yanga
|
No comments:
Post a Comment