Najiuliza Tu Lakini! Kuhusu Shimo hili Eneo la Jankisheni Mjini Ngara,Mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 22, 2018

Najiuliza Tu Lakini! Kuhusu Shimo hili Eneo la Jankisheni Mjini Ngara,Mkoani Kagera.

Moja ya chanzo kikubwa cha ajali za barabarani ni ubovu wa barabara hasa mashimo yanayochimbika na kuachwa kwa muda mrefu bila kufukiwa. Mashimo haya yamekuwa yakisababishwa na magari yenye uzito mkubwa na wakati mwingine kiwango hafifu cha barabara iliyotengenezwa.

Magari mengi yamekuwa yakipata ajali baada ya magurudumu kupasuka na gari kukosa mwelekeo baada ya kutumbukia kwenye shimo. 

Wakati mwingine ajali hizi zimekuwa zikitokea wakati madereva wakijaribu kukwepa mashimo hayo.

Lakini, Je, kama ni uzembe wa madereva kwa nini baada ya ajali kutokea mashimo hayo yamekuwa yakifukiwa na barabara kurekebishwa mara moja?. 

Kwa nini shimo lisiposababisha ajali linaweza kudumu hata kwa mwaka mzima barabarani?

NAJIULIZA TU LAKINI HILI SHIMO HAPA ENEO LA JANKISHENI MJINI NGARA .





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad