Aua Mke wake kwa Kisu kisa Mgogoro wa Kifamilia -Wilayani Kasulu,Kigoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 22, 2018

Aua Mke wake kwa Kisu kisa Mgogoro wa Kifamilia -Wilayani Kasulu,Kigoma.

Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Mbonimpaye Linus mkazi wa kijiji na kata ya Kalela wilayani Kasulu mkoani Kigoma, amefariki baada ya kuchomwa kisu tumboni na mume wake kutokana na migogoro ya kifamilia iliyokuwepo baina yao.

Akizungumzia tukio hilo Ndugu wa marehemu Bi. Sadasia Linus amesema tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita wakati mwanaume huyo akimfuatilia mke wake arudi nyumbani baada ya ugomvi kutokea na kusababisha mwanamke huyo kumkimbia mume wake na kurundi kwao.

Amesema mwanamke huyo akiwa njiani akimsindikiza mume wake baada ya kutoka nyumbani kwao na mwanamke, walipofika njiani alimkamata na kumchoma kisu tumboni kilichosababisha apoteze maisha papo hapo.

Diwani wa kata ya Kalela Bi. Dolisia Solomoni amelaani tukio hilo na kuitaka jamii kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi wakati mtuhumiwa akiendelea kutafutwa ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad