
![]() |
|
Gari
iliyohusika kwenye ajali hiyo ni namba T167 DTC aina ya Flight liner ambayo
ilikuwa na Trailer namba T 960 ALS. Hili gari ni mali ya Petromac Africa Dar es
salaam.
Gali iliacha
njia na kupinduka ambapo ililipuka na kusababisha moto mkubwa uliopelekea vifo
vya watu wawili ambao ni wanaume.
Uchunguzi wa
jeshi la Polisi wa awali baada ya kufatilia kwenye mzani wa Singida, gari
ilipimwa mzani wa Singida saa moja na dk 27 asubuhi dereva alikua anaitwa
Erasto Abedi Rusazi na alikuwa na tingo msaidizi wake anayeitwa Ramadhani
Hashim Ramadhini wote ni Wakazi wa Tabata Dar Es Salaam.
RPC Deborah
Magiligimba, ametoa wito kwa madereva watii sharia za barabarani ili kuepusha
ajali.
|









No comments:
Post a Comment