
![]() |
|
Ndogoni alisema
kwa waliosoma Jiografia, mchakato huo ni kama ule wa kugawanywa kwa mabara
saba, “Zile nguvu za kupasuka kwa miamba hadi yakawepo mabara saba duniani bado
zinaendelea. Mkondo huu wa Bonde la Ufa, ulianzia Kaskazini mwa Afrika katika
nchi za Djibouti, Kenya mpaka Kusini mwa Tanzania.”
Alisema
mkondo wa kwanza upo Ethiopia na kwa upande wa Kenya kuna miwili ambayo mmoja
ndio uliopita hadi katika baadhi ya maeneo ya Tanzania kama Manyara, Singida,
Iringa na Mbeya.
Alisema kasi
ya maeneo hayo kujitenga ni milimita 0.1 Kusini mwa Afrika na milimita 6.5
Kaskazini mwa Afrika na kwamba Tanzania ipo katikati ya maeneo hayo.
“Kumeguka
huku kwa bara la Afrika kunaleta wasiwasi kwa sababu kunatokea katika makazi ya
watu,” alisema.
|
![]() |
|
Dk James
Hammond wa Idara ya Sayansi na Uhandisi kutoka Chuo cha Imperial cha London
alinukuliwa na jarida la mtandaoni la Mail & Guardian akisema, “Katika
miaka milioni kadhaa ijayo, shughuli hii itakamilika na kuigawa Afrika mara
mbili, na kuunda bahari mpya hapo katikati.
Ukitumia jiografia ya sasa, bara
hilo jipya litashirikisha Somalia, nusu ya Ethiopia, Kenya na Tanzania.”
Baadhi ya
wanajiolojia wanakadiria kwamba huenda mpasuko huu ukayabeba pia mataifa ya
Uganda, Rwanda, Burundi na maeneo ya Malawi na Msumbiji.
Hivi
karibuni, maofisa wa Mamlaka ya Taifa ya Barabara Kenya (KeNHA) wakishirikiana
na mkandarasi kutoka China anayejenga reli ya kisasa, walifika katika bonde
hilo kuziba baadhi ya nyufa.
Baada ya
uchunguzi, ilibainika kwamba hali hiyo ilitokana na shughuli ya kijiolojia
chini ya ardhi ambayo ilihusisha mvutano wa vipande vikubwa vya ardhi.
Siku chache
baadaye, ufa huo uliendelea kupanuka na kuathiri barabara hiyo tena jambo
lililosababisha magari yenye kubeba mizigo mizito kushindwa kupita. Pia ufa huo
ulianza kuathiri nyumba za wakazi.
“Mkandarasi
na wahandisi wako hapo kwa sasa na watabaki ili kufuatilia yanayojiri kutokana
na shughuli za kivolkano ambazo zilisababisha ufa huo,” naibu mkurugenzi wa
mawasiliano wa Kenya, Charles Njogu alisema baada ya ukarabati huo mara ya
kwanza.
|








No comments:
Post a Comment