Taifa Stars yawafumua Wasakata Sebene 2-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 27, 2018

Taifa Stars yawafumua Wasakata Sebene 2-0.

Shiza Kichuya na Mbwana Samatta.

 Kikosi cha Tanzania ama Taifa Stars kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Taifa jioni ya leo March 27, 2018.

Mechi hiyo ya kalenda ya FIFA ilikuwa na mashambulizi ya zamu kwa timu zote mbili haswa katika kipindi cha kwanza kilichotawaliwa zaidi na wenyeji Taifa Stars.

Taifa Stars ilianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 74 kupitia kwa Mshambuliaji anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, kufuatia kazi nzuri ya Shiza Kichuya aliyepiga krosi safi kushoto mwa Uwaja na kumkuta Samatta ambaye bila ajizi akapiga mpira kwa Kichwa.

Dakika ya 86, Shiza Kichuya alioongezea Taifa Stars bao la pili kwa shuti kali la mguu wa kushoto, baada ya kutengenezewa pasi murua na Mbwana Samatta.
Ushindi huo unarejesha furaha na matumaini kwa Watanzania, baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Algeria kwa jumla ya mabao 4-1 ugenini.

DR Congo ni timu bora Afrika, inashika nafasi ya tatu nyuma ya Tunisia na Senegal, ipo nafasi ya 39 katika viwango vya Fifa vya mwezi Machi 2018 hivyo Stars imepata matokeo dhidi ya timu bora Afrika na Duniani.

Hadi sasa  Tanzania ipo nafasi ya 146 katika viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi machi 2018 ikiwa inapambana kusogea nafasi za juu kwa kucheza mechi zakirafiki za kimataifa dhidi ya timu ambazo zipo  katika nafasi za juu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad