![]() |
| Mkuu wa Polisi wilayani Ngara Abeid Maige akielezea mafanikio ya Kombe la Polisi Jamii 2018 kuwa yamekuza mahusiano kati ya Polisi na Jamii kupitia kauli mbiu ya KATAA UHALIFU,FICHUA WAHALIFU na jumla ya 18 zilishiriki mashindano hayo. |
![]() |
|
Kikosi cha Mabingwa
wa Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara Rulenge Stars.
|
![]() |
|
Kikosi cha Veterani FC kilichofungwa na Rulenge Stars wakati wa fainali ya Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara .
|

![]() |
|
Hili Kokoto aiseeee uwanjani Kokoto-uwanja wa wilaya ya Ngara mmmmmmmm''Mpira wa fainali huu , Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara.
|
![]() |
|
Golikipa wa Veteran FC mtumishi wa Benki ya NMB Tawi la Ngara aliibuka Bora wa Mashindano ya Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara na kuondoka na zawadi ya fedha 20,000/. koshoto kwake ni Mkuu wa Jeshi wa Polisi wilayani humo Abeid Maige na kulia ni Vedastus Tibaijuka,Katibu Tawala wilaya.
|

![]() |
Shuja wa mchezo huo ni Elias Jevent ambaye aliifungia timu yake mabao hayo yote
mawili na kumfanya kuibuka mfungaji bora wa mashindano kwa kufikisha mabao 7 na
kuondoka na zawadi ya fedha taslimu 20,000/.
Rulenge Stars kwa Kuibuka Bingwa ,amekabidhiwa zawadi yake na Mgeni rasmi
Mwenyekiti wa michezo wilaya na Katibu tawala wilaya ya Ngara mkoani Kagera
Vedastus Tibaijuka Ng’ombe mnyama ,Kikombe na Mpira mmoja huku Veteran FC
wakizawadiwa Mbuzi mnyama na Mpira mmoja wakati washindi wa tatu,Nyakariba FC
wakizawadiwa Mbuzi mmoja na Mpira mmoja baada ya kuibuka timu yenye nidhamu.
|
![]() |
|
Zawadi ya Mbuzi mnyama za Washindi wa Pili Veteran FC na Nyakariba FC washindi wa 3 wa Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara.
|
![]() |
|
Zawadi ya Bingwa wa Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara Rulenge Stars baada ya Kumfunga Veterani FC bao 2-0 katika fainali uwanja wa Kokoto Jana March 25,2018.
|
![]() |
|
Mwenyekiti wa Veterani FC Jose Sinzobakwila akipokea zawadi ya mpira na mbuzi wao baada ya kuwa washindi wa pili wa Polisi Jamii Cup 2018 wilayani Ngara.
![]() |



















No comments:
Post a Comment