![]() |
|
Mashabiki wa
FC Barcelona hupenda sana mchezo wa soka
Klabu ya FC
Barcelona imefahamika sana duniani kutokana na soka na imeonekana kuchukua
msimamo katika mjadala kuhusu uhuru wa jimbo la Catalonia nchini Uhispania.
Bendera na
rangi za klabu hiyo zimekuwa zikitumiwa katika maandamano ya kuunga mkono uhuru
wa jimbo hilo - kupitia kura ya maoni ambayo ilikuwa imeharamishwa na mahakama
ya Uhispania mjini Madrid.
Swali ambalo
wengi wamekuwa wakijiuliza ni hatima ya klabu hiyo ya jiji la Barcelona, jiji
kubwa zaidi Catalonia, iwapo jimbo hilo litafanikiwa kujitenga.
Je,
wataendelea kucheza La liga?
Mashabiki
wataendelea kufurahia mechi za utani wa jadi za El Clásico kati ya Barça na
mahasimu wao wakuu Real Madrid?
Katika mechi
hizo, Real Madrid wanaongoza wakiwa na mechi 95 ambazo wameshindwa dhidi ya 91.
Wanaosimamia
FC Barcelona wanasisitiza kwamba wao si wanasiasa; na kwamba rasmi klabu hiyo
haina msimamo kuhusu uhuru wa jimbo hilo.
Aidha,
hawajataka kujihusisha katika mjadala kuhusu ligi ambayow atashiriki Catalonia
wakijiondoa kutoka Uhispania.
|
![]() |
|
Barcelona
imekubali mikutano ya kuunga mkono uhuru kuandaliwa uwanjani Camp Nou
Mwaka 2014
hata hivyo FC Barcelona walijiunga na Mwafaka wa Taifa wa Haki ya Kuamua, kundi
lililojumuisha vyama vya kisiasa na mashirika ya kijamii ambayo yalikuwa
yanaunga mkono kura ya maoni ya kujitenga kwa Catalonia.
Klabu hiyo,
siku chache kabla ya kufanyika kwa kura hiyo baada ya polisi wa Uhispania
kuanza kuwakamata maafisa wa serikali ya Catalonia, ilitoa taarifa ya kisiasa
na kusema inatetea "demokrasia, uhuru wa kujieleza, na uhuru wa kuamua
mustakabali wa taifa".
FC Barcelona
wanaonekana kuamini kwamba wenyewe ndio wataamua ni ligi gani wataendelea
kucheza.
Hata
Catalonia ikijitenga kutoka kwa Catalonia, Barçelona wanaamini Wahispania
hawataacha kutazama mechi za El Clásico.
"Tutasalia
katika ligi moja na Espanyol," alisema naibu rais wa FC Barcelona Carles
Villarubà mapema mwezi uliopita akizungumzia klabu ya pili kwa umaarufu zaidi
mjini Barcelona, ambayo mashabiki wake wengi huunga mkono kusalia Uhispania.
Lakini
Javier Tebas, rais wa shirikisho la Uhispania linaloandaa La Liga alijibu:
"Barcelona hawawezi kuamua watachezea soka wapi iwapo shughuli ya uhuru
itakamilishwa Catalonia."
|
![]() |
|
Barcelona's trophies.
|
![]() |
|
Duru katika
klabu hiyo zimeambia BBC kwamba hakutakuwa na taarifa zozote rasmi kwa sasa
kuhusu hatima ya klabu hiyo.
Lakini duru
hizo zinasema: "Iwapo Catalonia watafanikiwa kujitenga, klabu hiyo
itahitajika kuzingatia maoni ya wanachama wake kabla ya kufanya uamuzi huo
muhimu.
"Pili,
na kwa heshima zote, tunaamini kwamba sisi ni nembo miongoni mwa zinazoongoza
katika soka duniani na ligi yoyote ile inaweza kufurahia sana kuwa nasi, ikiwa
ni pamoja na Ligi ya Uhispania."
Gabriel
Rufián, mwanachama wa Chama cha Republican cha Mrengo wa Kushoto cha Catalonia amesema
uwezekano wa Barça kuendelea kucheza ligi ya Uhispania hauwezi kuwa na tofauti
yoyote na Monaco ambao hucheza Ligi Kuu ya Ufaransa ilhali nchi yao si sehemu
ya Ufaransa.
Ni wachache
sana ambao wako tayari kufikiria uwezekano wa kuwa na ligi kuu ya Catalonia
ambayo bila shaka itatawaliwa na Barça iwapo itaundwa.
Uwezekano wa
Lionel Messi kuwakabili mabeki wa klabu ambazo hazina uzoefu mkubwa katika ligi
Catalonia, iwapo kutakuwa na ligi kama hiyo, haujawaingia vyema akilini watu
wengi.
"Siwezi
kufikiria La Liga ya Uhispania bila Barcelona," mkufunzi mkuu wa Real Madrid
Zinedine Zidane anasema.
"Kama
shabiki wa kandanda na michezo kwa jumla siwezi kulifikiria jambo kama
hilo."
Source-BBC Swahili.
|









No comments:
Post a Comment