Naibu Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
Selemani Jafo akitoka kukagua ujenzi wa choo cha walimu katika shule ya msingi
Chang’ombe ‘B’ wakati wa ziara yake aliyoifanya katika kata ya Chang’ombe.
Naibu Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi),
Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa wilaya nchini kuhakikisha wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu wanakwenda kuanza shule huku
akiwasisitiza wazazi watakaoshindwa kuwapeleka shule watoto hao wachukuliwe
hatua za kisheria.
Jafo ametoa
agizo hilo leo alipofanya ziara ya kukagua miundombinu mbalimbali katika shule
za msingi, Chadulu, Chang’ombe A na B, Manispaa ya Dodoma.
Katika ziara
yake ya kukagua maagizo aliyoyatoa kwenye shule hizo kuhusu masuala ya
miundombinu, Jafo amesema “Sisi kama
serikali hatutaki mtoto akose elimu hasa katika kipindi hichi ambacho serikali
imeamua kuelekeza nguvu za kutosha kwenye elimu kwa ajili ya watanzania.”
Ameongeza
“Kwa mzazi ambaye mtoto wake atabainika hajaenda shule na kupewa kazi zingine
kama kuendesha bodaboda hatua za kisheria zichukuliwe mara moja,”.
Pamoja na hayo, Jafo amekemea tabia ya wazazi
kutotilia mkazo masuala ya elimu na kuwakabidhi watoto wao kuendesha bodaboda
kama ajira yao badala ya kuwapeleka shule na kuwataka kuhakikisha wanawanunulia
mahitaji yote ya shule.
Aidha
amesema serikali haitarajii kuna vijana waliochaguliwa wakishawishiwa na wazazi
kufanya vibaya kwenye mitihani kutokana na elimu kuwa ni bure.
Akizungumzia
kuhusu watoto walioandikishwa kuanza kusoma elimu ya awali na msingi, Jafo
amesema kumekuwepo na mwitikio mkubwa katika suala la uandikishaji watoto hao
na linatokana na uwepo wa elimu bure.
Hata hivyo,
amesema shule nyingi idadi ya wanafunzi imeongezeka zaidi na kwa serikali ni
faraja kuona watanzania wengi sasa wanapata elimu huku akiwataka wazazi
wahakikishe watoto walioandikishwa wanahudhuria shule ipasavyo na wakurugenzi kuendelea kuweka mazingira
bora ya kujifunzia na kufundishia.
Kadhalika,
Jafo ameridhishwa na ukarabati wa miundombinu mbalimbali kwenye shule hizo huku
akiwaahidi walimu kuwa serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufundishia
ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
|
Thursday, January 12, 2017
Ma-DC waagizwa kuwachukulia hatua za Kisheria Wazazi wasiopeleka Watoto Shule.
Tags
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MATUKIO
Labels:
MATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment