Dereva endesha kwa Umakini sana ukifika eneo hili la K9 –Ngara,Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 09, 2016

Dereva endesha kwa Umakini sana ukifika eneo hili la K9 –Ngara,Kagera.

Eneo hili la K9 ambalo lina mteremko mkali-Barabara ya Benaco-Ngara lipo katika kijiji cha Kasharazi  wilayani Ngara mkoani Kagera ambapo ajali zinazotokea nyingi zikihusishwa na kupoteza mfumo wa breki na kupinduka.


Kwa wiki ya Agosti 29 hadi Septemba 01, jumla ya Watu wanne wamefariki Papo hapo  na mwingine kujeruhiwa baada ya kupata ajali ya gari/Lori walilokuwa wakisafiria kwenda nchi Jirani ya Burundi ambapo gari walilokuwa wakisafiria kupoteza mfumo wa breki na kupinduka.

“Nitoe wito kwa madereva wakifika eneo hili kufuata sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika sambamba na TANROAD MKOANI KAGERA kulitazama eneo hili la K9 kwa kuliwekea ALAMA zenye kuonesha hatari ya mteremko huo ili Madereva wanaopita barabara hii iwe vyepesi kwao kuona alama hizo , kuziheshimu na kuchukua tahadhali ya Mapema.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad