|
Mhe. Kijuu alimweleza
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa tetemeko hilo lilisababisha vifo vya wananchi
16, majeruhi waliolazwa katika Hospitali mbalimbali zilizoko kwenye mkoa wa
Kagera ni 170, Majeruhi waliotibiwa na kuruhiusiwa ni 83 na jumla ya majeruhi
wote ni 253.
Aidha nyumba za makazi
zilizoanguka ni 840, nyumba zilizopata nyufa ni 1,264 na majengo ya taasisi yaliyoripotiwa kuanguka ama
kupata nyufa ni 44.
Aidha, Mkuu wa Mkoa
alimweleza Mhe, Majaliwa kuwa mara baada ya tetemeko hilo kutokea uongozi wa mkoa
ulichukua hatua za haraka kwa kuokoa wananchi na kuwapeleka hospitali
mbalimbali kwa ajili ya matibabu. Pili, baadhi ya wananchi wenye nyumaba
zilizoathirika walipatiwa makazi ya muda na kuwahamasisha kusaidiana wao kwa
wao kupeana hifadhi. Mwisho Mkoa
unaendelea na tathimini ya athari na hasara zilizosababishwa na tetemeko hilo.
Agizo la Waziri Mkuu, Mkoa
chini ya Mwenyekiti wa kamati ya Maafa ya mkoa ambaye ni Mkuu wa Mkoa pia na
Maafisa kutoka kitengo cha Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu waendelee kufanya tathmini ya kina ya kubaini
athari na hasara za tetemeko hasa kwa kuanza na sehemu zinazohitaji huduma ya
haraka kama shule mbili za Sekondari za Ihungo na Nyakato ili Serikali iweze
kusaidia mara baada ya kupata tathimini ya hali halisi ya maafa.
|
No comments:
Post a Comment