|
Real Madrid,
Mabingwa wa Ulaya, wakicheza bila ya Mastaa wao wakubwa Cristiano Ronaldo,
Gareth Bale, Toni Kroos na Pepe,walitangulia kufunga Bao Dakika ya 21 kwa Bao
la Chipukizi Marco Asensio Willemsen aliekuwa akicheza Mechi yake ya kwanza
kabisa.
Sevilla
walisawazisha Dakika ya 41 kwa Bao la Franco Vazquez.
Kipindi cha
pili cha mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Larkendal nchini Norway kilianza
kwa kasi huku Sevilla wakionekana kuliandama zaidi lango la Madrid.
|
Konoplyanka
aliipatia Sevilla goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Sergio Ramos
kufanya madhambi kwenye eneo la hatari.
Baada ya bao
hilo Real Madrid waliliandama lango la Sevilla kama nyuki lakini ukuta wa mabingwa
hao wa Europa ulikuwa imara kuondosha hatari zote hadi dakika 90 za mtanange
huo zilipomalizika ndipo katika dakika tatu za nyongeza Ramos akaisawazishia
Madrid.
Mechi hiyo
ilikwenda katika muda wa nyongeza wa dakika 30 ambapo katika dakika ya 28,
Danny Carvajal aliipatia Madrid bao la tatu na la ushindi hivyo kutawazwa kuwa
mabingwa wa kombe hilo.
|





No comments:
Post a Comment