LIGI KUU VODACOM 2015/2016 :-Taswira Picha Yanga SC ikitawala Tuzo za Ubora kwa Juma Abdul,Kamusoko na Kocha Bora. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 18, 2016

LIGI KUU VODACOM 2015/2016 :-Taswira Picha Yanga SC ikitawala Tuzo za Ubora kwa Juma Abdul,Kamusoko na Kocha Bora.

IMG_0389
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Mwigulu Nchemba (kulia) akimkabidhi Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara 2015/2016, Juma Abdul (kushoto) hapo Jana July 17, 2016, hoteli ya Double Tree By Hilton.

Beki wa Yanga SC, Juma Abdul Jaffar Mnyamani ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/2016.

Katika sherehe za utoaji wa tuzo hizo Jana July 17, 2016,usiku kwenye ukumbi wa Double Tree Hotel By Hilton, Masaki, Dar es Salaam, Abdul ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars amewashinda beki mwenzake, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba SC na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shizza Kichuya.

Na kwa ushindi huo, Abdul mbali na kukabidhiwa taji na mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, pia amezawadiwa fedha Sh Milioni 9.2.

Tuzo hizo ni Mabingwa, Makamu Bingwa, Mshindi wa tatu, Mshindi wa nne, timu yenye Nidhamu, Mfungaji bora, Mchezaji bora wa Ligi, Kipa bora, Kocha bora, Mchezaji bora chipukizi, Mchezaji bora wa kigeni, Goli bora la msimu na Mwamuzi bora,msimu  ambao ulimalizika Mwezi Mei kwa Yanga SC kuibuka Mabingwa wa Ligi hiyo kuu Vodacom Tanzania bara na kutwaa taji lao kwa mara ya 26 katika historia.

Kwenye mabano ni kiasi cha fedha ambacho washindi wa tuzo wamepata kutoka kwa mdhamini wa ligi Tanzania bara, tuzo zilitolewa kwa washindi kama ifuatavyo,-

IMG_0308
Mshindi wa nne: Tanzania Prisons ya Mbeya (Tsh.23,241,635)


IMG_0310
    2. Mshindi wa tatu: Simba SC ya Dar es Salaam (Tsh. 29,052,044)


IMG_0313
3. Mshindi wa pili: Azam FC ya Dar es Salaam (Tsh. 40,000,000)


IMG_0318
4. Bingwa wa ligi kuu 2015/2016: Yanga SC ya Dar es Salaam  (Tsh. 40,672,861)


IMG_0323
5.Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa nchini, Mohammed Hussein 'Mmachinga' akimkabidhi tuzo ya Mfungaji bora wa msimu wa 2015/2016, Amis Tambwe Tsh. 5,742,940)-alifunga magoli 21 magoli mawili mbele ya mpinzani wake Hamisi Kiiza aliyefunga magoli 19.


IMG_0333
6. Timu yenye nidhamu: Mtibwa Sugar ya Morogoro (Tsh. 17,228.820)


IMG_0336
7. Rais wa zamani wa TFF, Wakili Said El Maamry (kulia) akimkabidhi Ngole Mwangole tuzo ya Mwamuzi bora (Tsh. 5,742,940).

Walioingia katika kinyang’anyiro hicho ni Anthony Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab Mrope.

IMG_0357

IMG_0356
Kipa bora wa zamani, Mwameja Mohammed (kushoto) akimkabidhi tuzo ya Kipa Bora wa Ligi Kuu, Aishi Manula (kulia) Azam FC (Tsh. 5,742,940)
Majina yaliyopendekezwa kuwania tuzo hiyo ni Aishi Manula (Azam FC) Beno Kakolanya (Tanzania Prisons) na Deogratius Munishi (Yanga SC).


IMG_0344
    Hans van der Pluim (Yanga SC (8,000,000) akipunga mkono baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya Kocha Bora wa Ligi Kuu. 

Waliokuwa wakipambana kuwania tuzo ya kocha bora wa msimu uliopita ni Hans Van Pluijm (Yanga), Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na Salum Mayanga (Tanzania Prisons).


IMG_0363
Rais wa TFF, Jamal Malinzi akimkabidhi mfano wa Hundi, Thabani Kamusoko (Yanga) (Tsh. 5,742,940),aliyeongozana na mkewe Bongile Sibanda (kushoto) na mwanawe, Shanna Lee, Tuzo ya Mchezaji bora wa kigeni . 

Waliongia kwenye orodha ya tuzo ya mchezaji bora wa kigeni ni Donald Ngoma (Yanga), Thabani Kamusoko (Yanga) na Vincent Agban (Simba).


IMG_0381
Ofisa Mkuu wa Masoko wa Vodacom, Ashutosh Tiwary akimkabidhi Mohammed Hussein 'Tshabalala' (Simba SC )  (Tsh. 4,000,000) mfano wa Hundi kwa kuwa Mchezaji Bora Chipukizi.

Waliokuwa wakiwania tuzo hiyo ni Farid Mussa (Azam), Mohamed Hussein (Simba), Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).


IMG_0427
    Washindi wote wa tuzo za Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara 2015/2016, kutoka kulia Tshabalala, Kamusoko, Tambwe, Juma Abdul, Aishi Manula na Hajib.

Goli bora la msimu 2015/2016: tuzo imekwenda kwa Ibrahimu Ajib (Simba SC (Tsh. 3,000,000).

Ajib alikuwa akipambana na Amis Tambwe (Yanga) katika kuwania tuzo ya goli bora la msimu 2015-16.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad