MATOKEO/RATIBA VPL 2015/2016:-Simon Msuva wa Yanga SC aishusha Simba SC Kileleni mwa Ligi Kuu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 16, 2016

MATOKEO/RATIBA VPL 2015/2016:-Simon Msuva wa Yanga SC aishusha Simba SC Kileleni mwa Ligi Kuu.


Mabingwa wa Ligi ya Vodacom Tanzania bara ,Timu ya Yanga SC imerejea kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuifunga Mtibwa Sugar kwa goli 1-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo April 16, 2016.

 Yanga SC ilienguliwa kileleni mwa ligi na mahasimu wao Simba SC takribani mwezi mmoja ulipita lakini wamerejea kwenye nafasi yao kufuatia kushinda mechi zao za viporo.

Mechi hiyo ya kiporo ilipoteza ladha kutokana na uwanja kujaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha siku ya leo huku wachezaji wa timu zote wakianguka mara kwa mara na mipango ya timu zote ikishindwa kukamilika.

Bao pekee la ushindi limefungwa na Simon Msuva dakika ya 48 kipindi cha pili kwa kiki ya chinichini aliyoiachia akiwa nje ya eneo la hatari na kumshinda mlinda mlango wa Mtibwa Sugar Said Mohamed.

Yanga SC inafikisha pointi 59 baada ya kucheza mechi 24 na kuwateremshia nafasi ya pili mahasimu wao Simba SC wenye pointi 57 za mechi 24 na Azam FC wakiwa wa tatu kwa Pointi 55 kwa michezo 24.

Hata hivyo, Simba SC wanaweza kurejea kileleni kesho wakiifunga Toto Africans kwenye Uwanja huo huo katika mchezo mwingine wa ligi hiyo.

Matokeo ya mechi Nyingine za leo Jumamosi Aprili 16,2016.

Coastal Union 1 – 0  JKT Ruvu  

Ndanda FC 2 - 0 Kagera Sugar

Ratiba VPL 2015/2016.

Jumapili Aprili 17,2016.

Simba SC v Toto Africans 

Jumatano Aprili 27,2016.

Azam FC v Majimaji

Yanga v Mgambo JKT      

Jumamosi Aprili 30,2016.

Toto Africans v Yanga       

Simba SC v Azam FC       

African Sports v Coastal Union   

Mwadui FC v Stand United

Mtibwa Sugar v Mbeya City

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad