RC Kagera –‘’Sipo tayari Kuruhusu Zao la Kahawa liuzwe kwa Njia za Magendo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 24, 2018

RC Kagera –‘’Sipo tayari Kuruhusu Zao la Kahawa liuzwe kwa Njia za Magendo.

Chama cha ushirika Wilayani Ngara Mkoani Kagera Ngara Farmers kimetengewa Jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni 1 na milioni 226 kwa ajili ya ununuzi wa zao la kahawa. 

Kauli hiyo imetolewa na Afisa kilimo Wilaya ya Ngara Bw Costantine Mdende akiwataka Watendaji wa Vijiji na Kata kusimamia na kuwaelimisha wananchi juu ya maelekezo yaliyo tolewa na Serikali kuhusu  utaratibu unao takiwa wakati wa ununuzi na uuzaji wazao  hilo.

Aidha Bw.Mdende ameongeza kuwa Mwananchi yeyote atakaye uza kahawa yake bila kuzingatia maelezo yaliyo tolewa na Serikali   hatua kali za kisheria zita chukuliwa dhidi yake ikiwemo kwa mtu Binafsi faini yake ni kuanzia milioni 10, Kampuni ni kuanzia milioni 100 sambamba na Kifungo.

Wakizungumza na Radio Kwizera baadhi ya Watendaji wameahidi kuzingatia maelekezo waliyopewa huku wakisema wanaenda kuwaelimisha Wananchi juu ya madhara yanayo weza kujitokeza endapo watauza kahawa bila kuzingatia maelekezo ya Serikali.
Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Kagera alionya kuhusu zao la Kahawa akisema, Msimamo wangu mimi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu Kuhusu zao la Kahawa ni kuwa sipo tayari kuruhusu zao la kahawa liuzwe kwa njia za magendo. 

Nitahakikisha namchukulia hatua kali za Kisheria yeyote yule atakayeweka kikwazo kwa Mkulima kuuza kahawa yake kupitia Vyama vya Ushirika.

Viongozi wa Vyama vya Ushirika kuweni makini na kila shilingi ya mkulima Mtambue kuwa Serikali ipo kazini inafuatilia kila kitu kinachofanyika ndani ya Vyama vyenu. Hatutasita kuchukua hatua muda na wakati wowote mkicheza na fedha ya Wakulima. 

Mtazamo na furaha yangu nataka kuona Mkulima anatajirika, ana fedha mfukoni kutokana na zao la Kahawa na lazima Vyama viwe mkombozi wa wakulima na si wanyonyaji wa Wakulima.” Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad