Waziri wa
Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla na Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii, Japhet Hasunga wakipongezwa na wabunge mbalimbali baada ya bajeti ya
wizara yao kupitishwa na Bunge May 23,2018.
Pori la Akiba Burigi lina ukubwa wa kilomita za mraba 2,941
katika wilaya za Karagwe, Muleba na Ngara mkoani Kagera, wakati Pori la Kimisi
likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 1,030 katika wilaya za Ngara na Karagwe
mkoani humo.
Pori la Akiba Biharamulo lina ukubwa wa kilomita za mraba 731
katika wilaya ya Muleba mkoani Kagera na wilaya ya Chato mkoani Geita, huku
Pori la Akiba Ibanda
likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 200 na Pori la Akiba Rumanyika kilomita za mraba 800
katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera.
Mapori haya yapo katika ukanda muhimu wa kuunganisha watalii kutoka ikolojia za Magharibi na Mashariki ambapo uwanja wa ndege wa Chato utakuwa muhimu katika kutoa mawasiliano.
Mapori hayo ambayo yanasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania
- TAWA sasa yatakuwa chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania - TANAPA
punde baada ya mchakato wa kuyapandisha hadhi kukamilika.
|
Picha ya
pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kigwangalla,
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga, Katibu Mkuu, Maj. Gen.
Gaudence Milanzi, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Aloyce Nzuki, Wakuu wa Idara, Vitengo
na Taasisi pamoja na wafanyakazi wa wizara hiyo baada ya bajeti ya wizara
yao kupitishwa na Bunge.
|
No comments:
Post a Comment