Mabasi saba
ya abiria yamekamatwa na kutozwa faini
kwa kosa la mwendokasi na kutofuata sheria za usalama barabarani huku
wakihatarisha maisha ya abiria.
Kamatakamata
hiyo ambayo imesimamiwa na Kamanda wa
kikosi cha usalama barabarani
Fotunatus Muslim akiwa na timu ya
viongozi na askari mkoa wa Morogoro
imefanyika usiku wa kuamkia leo leo September 16,2017.
Zoezi la
ukamataji mabasi hayo limefanyika eneo la Dumila Wilaya ya Kilosa mkoani hapa,
zoezi lilichukua takribani masaa mawili ambapo mabasi hayo yamezuiwa kuondoka
mpaka asubuhi huku yakitozwa faini.
Kamanda
Muslim amesema jeshi hilo halitakubali kuona maisha ya watanzania
yakipotea kutokana na uzembe wa baadhi
ya madereva.
Amesema kikosi hicho cha usalama barabarani kimeahidi
kupambana na madereva wa mabasi ya abiria hasa nyakati za usiku kwani ndio
wamekuwa wakiendesha kwa mwendokasi huku wakidai serikali muda huo inakuwa imelala.
Mabasi ya
abiria zaidi ya saba yanayofanya safari kati ya mkoa wa Mara (Musoma) Dar es
salaam, na Mwanza- Dar es salaam yamekaguliwa na kutozwa faini.
Muslim
amesema madereva wengi wamekuwa
wakifuata sheria za barabarani nyakati za mchana kwa kuhofia kukamatwa kutokana
na tochi zilizopo na inapofika nyakati za usiku madereva hao wamekuwa wakitumia
mwanya wa kuendesha kwa mwendo kasi.
Akizungumzia dhamira ya Polisi Muslim amesema ni kuwalinda raia na mali zao
na kuwataka askari wa usalama barabarani kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Amesema
doria ni endelevu na sasa itakuwa kwa nchi nzima kwa usiku na mchana huku
akiwataka madereva hao kuacha kudanganyika kwa madai kuwa tochi usiku hazifanyi
kazi usiku na kwamba tochi sasa zitakamata mpaka usiku.
"Nimekuja
na slogani ya Kamata hii ni kwa wale madereva wasiotii na kufuata sheria na
tutapambana nao kila wakati na nyakati zote na hiyo itasaidia abiria kusafiri
salama na matumizi ya barabarani kuwa bora," amesema kamanda Muslim
Mmoja wa
abiria aliyejitambulisha kwa jina la Leon Mwete aliyekuwa katika moja ya basi
yaliyokamatwa eneo hilo la Dumila amesema zoezi hilo ni zuri na linafaa
kuendelea.
Amesema hii
itapunguza ajali za barabarani na kwamba kwa sasa uendeshaji wa madereva wengi
ni mzuri ukilinganisha na zamani.
Naye kamanda
wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro Boniface Mbao ameeleza kuwa
yeye akiwa msimamizi mkuu ataendelea kusimamia na kufanya oparesheni za usiku
na mchana kama maelekezo yaliyotolewa.
|
No comments:
Post a Comment