Lowassa Kaachiwa Huru ......Taswira Picha Jinsi Alivyokamatwa - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 17, 2017

Lowassa Kaachiwa Huru ......Taswira Picha Jinsi Alivyokamatwa


Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea wa Urais 2015 kupitia CHADEMA, Bw.Edward Lowassa Jana January 16,2017  alikamatwa na jeshi la Polisi  wakati akiwa anaenda kwenye kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome na baadaye aliachiwa  huru ambapo taarifa za polisi zinadai kuwa walimzuia kwa sababu za kiusalama.

 Mbali na hivyo, Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi walioandamana kwenda kituo cha polisi baada ya Lowassa kukamatwa.

Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,ACP Lotson Mponjoli, amesema kuwa hawakuwa wamemkamata Edward Lowassa bali walikuwa wakijadiliana naye kuhusu usalama wake na jamii.




Kupitia kituo cha Television cha Azam wameripoti habari ya kukamtwa kwa Lowassa ambapo baadhi wa wananchi wameeleza ilivyokuwa.

"Tulikuwa kwenye msafara ya kumpokea Lowassa lakini tulipofika hapa stendi wananchi walitaka kuongea na Lowassa, kabla hata hajashuka kwenye gari askari walituvamia wakasema tuondoke moja kwa moja twende kituoni"- shuhuda

''Sikiliza mkasa mzima hapo chini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad