MADAWANI SHULENI:- Halmashauri zote zatakiwa kukamilisha Agizo la Rais Magufuli Ifikapo Mwezi Juni,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 26, 2016

MADAWANI SHULENI:- Halmashauri zote zatakiwa kukamilisha Agizo la Rais Magufuli Ifikapo Mwezi Juni,2016.

Na Daudi Manongi- MAELEZO.

Halmashauri  za Miji na Wilaya nchini zimekumbushwa kukamilisha zoezi la upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari ifikapo Juni 30 mwaka huu,2016 ili kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Rai hiyo imetolewa  leo,May 26,2016  na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi kuhusu uchakavu wa madarasa na ukosefu wa madawati unaozikabili shule za kinesi A na B zilizopo wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Suala la upungufu wa madawati na uchakavu wa madarasa ni changamoto ya kitaifa na kwamba lilishatolewa agizo na mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu halmashauri zote nchini kuhakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu kila mwanafunzi anaketi kwenye Dawati” Alisema  Kwandu.

Kwa mujibu wa Gwandu alisema Serikali ya awamu ya tano imepania kuinua kiwango na ubora wa elimu nchini kupitia mikakati na sera ya elimu bure nchini kote.

Aliongeza kuwa hatua hiyo imeibua changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi kujitokeza kwa asilimia kubwa na hivyo ni wajibu wa halmshauri hizo kukidhi mahitaji ya madawati ili wasome katika mazingira mazuri.

Mpaka sasa Serikali imeendelea kutoa pesa kwa ajili ya elimu bure nchini kote na kumekuwepo kwa changamoto mbalimbali kama upungufu wa walimu,madawati na madarasa ambapo serikali inafanya jitihada za kila namna ili kutatua changamoto hiyo

Akifafanua zaidi Gwandu alisema Serikali inaandaa harambee mbalimbali na kuongeza wigo wa utoaji wa vibali vya kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ili kutoa  nafasi kwa wadau mbalimbali wenye nia ya kufanya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad