JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA
WATOTO.
TAMKO KUHUSU
MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI LILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU
(MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO, TAREHE 25
JANUARI 2016.
Ndugu
Waandishi wa Habari,
Wizara yangu
inaendelea kutoa taarifa ya wiki kwa umma kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa
kipindupindu hapa nchini. Hadi kufikia tarehe 24 Januari 2016, jumla ya watu
14,608 wameugua ugonjwa huo, na kati yao watu 228 wamepoteza maisha kwa ugonjwa
huu. Njombe, Ruvuma na Mtwara ndiyo Mikoa pekee ambayo haijawahi kuripoti
mgonjwa yoyote wa kipindupindu, tangu mlipuko huu uanze mnamo mwezi Agosti
mwaka huu.
Kwa mujibu
wa Takwimu za kuanzia tarehe 18 hadi 24 Januari 2016, ni kuwa jumla ya Mikoa
ambayo imeripoti kuwa na wagonjwa ni 15 ambapo idadi ya wagonjwa 524 na vifo 10
vimeripotiwa.
Idadi ya
wagonjwa walioripotiwa wiki hii imepungua ukiliinganisha na idadi ya wiki
iliyoishia tarehe 17 ambapo kulikuwa na wagonjwa 621 na vifo 14 ambalo ni
punguzo la asilimia (16%).
Mkoa wa
Morogoro bado umeendelea kuripoti idadi kubwa zaidi ya wagonjwa ukilinganishwa
na Mikoa mingine, (Manispaa ya Morogoro 89, Halmashauri ya Morogoro 36, Mvomero
17), ukifuatiwa na mikoa ya Mwanza (Ukerewe 36, Nyamagana 19 na Ilemela 13),
Simiyu (Bariadi DC 29 na Bariadi municipal 23), Manyara (Simanjiro 48), Mara
(Musoma Manispaa 11, Musoma DC 8, Rorya 8 na Butiama 8), Geita (Geita DC 21 na
Geita TC 6) na Mbeya (Kyela 26).
Mikoa
mingine ambayo bado pia imeendelea kuripoti wagonjwa ni pamoja na Dodoma
(Wagonjwa 22), Arusha (21), Tabora (18), Singida (18), Lindi (12), Rukwa (7),
Kilimanjaro (6) na Kagera (2).SOMA ZAIDI TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI.
|
Monday, January 25, 2016
TAMKO:- Kuhusu Mwenendo wa Ugonjwa wa Kipindupindu Nchini Tanzania.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment