KAMPENI ZA UKAWA 2015:-Taswira Picha mkutano wa Edward Lowassa Mjini Sumbawanga. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 03, 2015

KAMPENI ZA UKAWA 2015:-Taswira Picha mkutano wa Edward Lowassa Mjini Sumbawanga.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Ikuo Malila, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais hiyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini, hapo jana Sepremba 2, 2015.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akizungumza wakati akitolea taarifa swala na ratiba ya Mikutano ya Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa (kushoto) uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini, jana Sepremba 2, 2015.Kulia ni Mke wa Mh. Lowassa, Mama Regina Lowassa.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akihutubia maelfu ya wananchi Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini, jana Sepremba 2, 2015 ambapo alitangaza kuanza kampeni zake kwa kutumia helikopta (chopa) nne ambazo zitatikisa anga katika mikoa yote nchini kuomba ridhaa ya wananchi kukichagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Alisema Tanzania nzima kuna majimbo ya uchaguzi 265 ambako Zanzibar yako 50 na Tanzania Bara 215.

Aliongeza kuwa siku za kampeni ni siku 60 mgombea urais Ukawa hawezi kufikia majimbo yote hivyo Chadema imeunda vikosi vinne vya askari wa mapambano ambavyo vitaundwa na wabunge makini na baadhi ya viongozi ambao watafanya kampeni nchi nzima kwa kutumia helikopta nne.

Aliwataja wabunge hao watakaounda kikosi hicho wanaomaliza muda wao kuwa ni Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Ezekiel Wenje (Nyamagana), David Silinde (Momba), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Mbeya Mjini), John Mnyika (Ubungo), Halima Mdee (Kawe) na yeye (Mbowe) ambaye ni wa Hai.

Vikosi hivi vitachana nchi nzima kwa kutumia helikopta kuanzia wiki ijayo, hivyo majimbo ambayo mgombea urais hatafika vikosi vitafika na maeneo mengine atakwenda mgombea mwenza,”alisema.


Sehemu ya Wananchi wa Mji wa Sumbawanga, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga, wakiishangilia Ndege iliyombeba Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati ikiwasili Uwanjani hapo,  Sepremba 2, 2015.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa, wakiwapungia mikono maelfu ya wananchi wa Sumbawanga Mjini, waliofurika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, jana Sepremba 2, 2015.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini, amesema anajua vizuri mahitaji na kero za watanzania na amewaomba watanzania kumpa dhamana ya kuleta mabadiliko ya kweli kwani uwezo huo anao na anachohitaji ni ushirikiano wao. 


 Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad