TAHARUKI:-Taswira Picha wakati Meli ya Mv.Serengeti ikipigwa na dhoruba ziwa Victoria kwa saa kadhaa leo August 17,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, August 17, 2015

TAHARUKI:-Taswira Picha wakati Meli ya Mv.Serengeti ikipigwa na dhoruba ziwa Victoria kwa saa kadhaa leo August 17,2015.


Kwa mbali ni muonekano wa Meli ya Mv. Serengeti iliyopigwa na dhoruba leo hii August 17, 2015 majira ya asubuhi, ikiwa imebakiza Kilometa chache kufika Bandari ya Bukoba,Mkoani Kagera.



Meli hiyo iliyokuwa ikitokea jijini Mwanza kuelekea mjini Bukoba ambapo ilikumbana na upepo mkali ndani ya ziwa victoria  na kushindwa kutia nanga katika bandari ya Bukoba nakupelekea nahodha wa meli hiyo kuirudisha majini mpaka upepo ulipo tulia ndipo ilifanikiwa kutia nanga katika bandari ya Bukoba majira ya saa tano asubuhi.

Nahodha wa meli hiyo Bembele Mwita amesema kuwa meli hiyo ilikuwa haina tatizo lolote la kiufundi bali upepo mkali ulikuwepo ndani ya ziwa Victoria ndio ulichangia kwa kiasikikubwa na kukwamisha meli hiyo na kushindwa kutioa nanga katika bandari ya Bukoba.



Hatimaye Meli ikafanikiwa kutia nanga katika bandari ya Bukoba,mkoani Kagera na abiria wote wako salama.


Nitakribani miezi miwili imepita meli ya Mv Serengeti ianze kufanya kazi kama mbadala wa meli ya Mv Victoria baada ya kusimamishwa kwa ajili ya matengenezo. 

Wakizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya meli hiyo kutia nanga katika bandari ya Bukoba baadhi ya wananchi wamesema meli hiyo ilianza kuyumba majini majira ya saa kumi na moja alfajiri hali ambayo imewatia wasiwasi ambapo wamekaa majini kwa zaidi ya saa sita ndipo walipofanikiwa kutoka majini huku wakiwa wanahali mbaya kisaikorojia.

PAPO KWA PAPO Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp  +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad