MAFANIKIO YETU:-Taswira Picha wakati Rais Kikwete akizindua Kivuko cha Mv Mafanikio na kuweka Jiwe la Msingi mradi wa nyumba za makazi NHC Shangani mkoani Mtwara - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 09, 2015

MAFANIKIO YETU:-Taswira Picha wakati Rais Kikwete akizindua Kivuko cha Mv Mafanikio na kuweka Jiwe la Msingi mradi wa nyumba za makazi NHC Shangani mkoani Mtwara

Sehemu ya kivuko cha Mv Mafanikio kilichozinduliwa Rais Dkt Jakaya Kikwete mapema leo August 9, 2015 kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu mkoani Mtwara. PICHA NA MICHUZI JR-MTWARA.

Rais Kikwete akizindua rasmi kivuko cha MV Mafanikio kwenye pwani ya mji wa Mtwara kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu muda huu mkoani Mtwara.

Rais Dkt.Jakaya Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko cha Mv Mafanikio kwenye pwani ya mji wa Mtwara kitachofanya safari kutokea Msemo kuelekea Msangamkuu muda huu mkoani Mtwara.Kivuko cha MV Mafanikio kina uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa ameambatana Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli mara baada kushuka kwenye kivuko cha Mv Mafanikio katika kata ya Msanga Mkuu-Mtwara vijijini mara baada ya kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete,kivuko hicho kina uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi  katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu pamoja na Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu akizungumza jambo na Rais  Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,Kulia ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakiondoka eneo la tukio mapema leo August 9, 2015 mchana.
Naibu Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi Mh.John Pombe Magufuli kabla ya uzinduzi wa Kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo mchana. 
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Jakaya Kikwete kabla ya uzinduzi wa kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo mchana,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh.Fatma Salum Ali.
Rais Dkt Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Fedha,Mh Mwigulu Nchemba ambaye pia alihudhuria sherehe hizo fupi uzinduzi wa kivuko cha Mv Mafanikio mkoani Mtwara mapema leo August 9, 2015 mchana.
 

 
 
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini waliofika kwenye uzinduzi wa kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3.
 
Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt Jonh Pombe Magufuli akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini baada ya uzinduzi wa  kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3,Dkt Magufuli amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete katika utawala wake ndani ya maiaka kumi amefanikiwa kujenga vivuko vipya 15 na vingine 7 vimekwishakarabatiwa na vinafanya kazi mpaka sasa.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini kuzindua kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3.

 
Mkuruegenzi Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza jambo mbele ya mgeni rasmi Rais Dkt Jakaya Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi kwa ujumla katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4.
PICHA NA MICHUZI JR-MTWARA.
 
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad