![]() |
|
Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Alvaro
Rodriguez.
UMOJA
wa Mataifa umetaka vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa kuhakikisha
vinatoa taarifa zao kwa usahihi kuhusu maandalizi ya uchaguzi na uchaguzi
wenyewe.
Kauli
hiyo imetolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa Dar es salaam, kufuatia taarifa
iliyochapishwa na jarida moja kwamba UN inataka kujitoa katika kusaidia
mandalizi ya uchaguzi nchini Tanzania.
Aidha
alisema kwamba si kweli kuwa Umoja wa Mataifa haujaridhishwa na mwenendo wa
maandalizi ya uchaguzi nchini Tanzania na kwamba Umoja huo utaendelea
kushirikiana na serikali na vyombo vingine vya uchaguzi kuhakikisha uchaguzi
unakwenda vyema.
Indian
Ocean Newsletter ya Julai 10 mwaka huu ilichapisha habari iliyoandikwa na
kichwa cha habari “State is facing electoral commissions negligence” na
kusema kwamba Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),
Bw. Alvaro Rodriguez, haridhishwi na mwenendo wa maandalizi ya uchaguzi na
uchaguzi wenyewe na kutishia kuondoa msaada wa mamilioni unaoratibiwa na UNDP
kutoka kwa wahisani mbalimbali.
Aidha
Julai 15, 2015, mtandao wa Jamii Forum ilitafsiri habari hiyo kwa
Kiswahili na kuitawanya kwa wasomaji wake..Taarifa ambayo sio sahihi iliyochapwa na Jamii forum hii hapa link
Ukweli ulivyo.
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini hajawahi kukutana wala kuzungumza na watu wa Indian Ocean
Newsletter .
Aidha taarifa zilizotolewa na kijarida hicho
na tafsiri yake iliyowekwa mtandao wa kijamii wa Jamii Forums hazikujengwa
katika ukweli.
Pia Umoja wa Mataifa utaendelea
kufanyakazi na mamlaka za Tanzania na wananchi wake na kuwa Uhusiano kati ya
Umoja wa Mataifa na mamlaka za uchaguzi nchini Tanzania na Jumuiya ya kimataifa
inayofadhili mradi wa DEP unawasilisha mahusiano muhimu miongoni mwa wadau
mbalimbali wanaotaka kuwapo na uchaguzi huru na wa amani.
Alisema katika makubaliano kuna kamati ya
mradi inayojumuisha wadau wote na ina wajibu kuongoza na kutoa mwongozo wa
utekelezaji mradi huo kimkakati.
Maamuzi ya mradi huo hufanywa na kamati hiyo
na kamati ya ufundi ya mradi iliyopo Bara na Zanzibar.
Kutokana na ukweli huo Umoja wa Mataifa
unavitaka vyombo vya habari vya kitaifa na Kimataifa kuhakikisha kwamba inatoa
taarifa za ukweli na za usahihi kipindi hiki cha maandalizi na uchaguzi
wenyewe.
|
![]() |
|
Biometric
Voter Registration (BVR) Machines operator, Kheri Mkali attends Rebeca Kimu at
Bunju A in Dar es Salaam yesterday during the trial registration. (LIBRARY
PHOTO|VENANCE NESTORY).
Background.
The Democratic Empowerment
Project is a three year project launched on the 12th of March 2013 and is
directly executed by UNDP with UN Women and UNESCO through a donor basket fund.
It follows two previous electoral support projects in Tanzania: the Electoral
Assistance Project of 2005 and the Election Support Project of 2010.
The USD
25m project has four main components, namely, a) supporting legal and
institutional reforms; b) support improvement of Electoral Management body’s
capacities(NEC and ZEC); c) promote inclusive participation in political and
electoral processes, and d) support national peace infrastructures.
More
specifically, the project has been supporting both NEC and ZEC to improve their
institutional capacity both in the context of the conduct of the voter
registration process (but not the provision of the BVR kits which is the
government’s responsibility) and the preparations for the 2015 general
elections.
DEP’s support has included technical and advisory services, staff
training, voter education and stakeholder engagement. Such stakeholders include
the Office of the Registrar of Political Parties, political parties, media,
civil society and groups representing women, youth and people with
disabilities.
So far DEP has supported and implemented most of these
activities either directly or via cooperation agreements with the electoral
management bodies who execute specific activities directly in line with their
mandate.
Issued
by: The Office of the UN Resident Coordinator and UNDP Resident
Representative – Mr. Alvaro Rodriguez
For more information,
please contactHoyce Temu-UN Communications Specialist at hoyce.temu@one.un.org or
Aine Mushi, UN Coordination Specialist at aine.mushi@one.un.org
Pata
Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori
inayonifikia wakati wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|







No comments:
Post a Comment