BREAKING NEWS:- Nyumba mali ya Bw Aron Rugamira imeteketea kwa moto katika Kitongoji cha Kumzenga kwenye mamlaka ya Mji wa Ngara Mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, June 27, 2015

BREAKING NEWS:- Nyumba mali ya Bw Aron Rugamira imeteketea kwa moto katika Kitongoji cha Kumzenga kwenye mamlaka ya Mji wa Ngara Mkoani Kagera.

Pichani juu na chini ni Muonekano wa Nyumba yenye thamani isiyotambulika mara moja mali ya Bw Aron Rugamira imeteketea kwa moto katika Kitongoji cha Kumzenga kwenye mamlaka ya Mji wa Ngara Mkoani Kagera leo June 27, 2015,majira ya saa saba mchana.

Miongoni mwa mashuhuda  wa tukio hilo Bw Moses Rusasa amesema moto huo umetokea kwenye chumba kilichokuwa hakijaunganishwa na nishati ya umeme na kwamba halijasababisha madhara ya kiafya kwa mtu yeyote hadi sasa na kwamba asilimia kubwa ya mali alizokuwa akimiliki zimeteketea kwa moto.


Kwa upande wake mmiliki wa nyumba hiyo Bw Aroa Rugamira akizungumza na Radio Kwizera iliyofika eneo la tukio, amesema tukio hilo wakati likitokea hakuwepo nyumbani kwake na alikuwa kwenye shughuli zake za Kijamii.
Pata Picha, Habari za Kisiasa, Kijamii, Kiuchumi na Michezo kila stori inayonifikia wakati  wowote ukijiunga na mimi kwa kubonyeza…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad