|
MTANZANIA.
Mkazi wa
Kata ya Buhare Manispaa ya Musoma, Helena Paulo mwenye umri wa miaka 21
amejifungua watoto pacha wa kike walioungana kifua na tumbo katika
hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mara.
Kutokana na
taarifa za watoto hao kusambaa mitaani,wananchi walimiminika hospitalini hapo
kushuhudia watoto hao waliozaliwa Januari 4 mwaka huu likiwa ni tukio la pili
baada ya lile la kwanza kutokea Agosti6 mwaka jana.
Akielezea
hali ya pacha mkunga wa zamu wa hospitali hiyo Elisifa Makala alisema
walimpokea mjamzito Helena January3 akiwa mwenye uchungu wa kawaida na
kuamua kumpumzisha kusubiri kujifungua kutokana na kutokua na tatizo lolote.
Alisema
ilipofika saa 8 usiku alianza kusikia uchungu ambapo alipewa msaada wa
kujifungua lakini alishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida kutokana na mtoto
kutanguliza miguu na kufanyiwa upasuaji ambapo waliwakuta watoto wakiwa
wameshikana.
MTANZANIA.
Watu 22
wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya jiji la Dar es salaam kwa makosa
mawili tofauti,likiwemo la kufanya biashara ya kuuza miili yao.
Akisoma
shtaka hilo mwedesha mashtaka Ramadhan Kalinga alisema watuhumiwa hao
walikamatwa maeneo ya Ubungo na kwamba walikua wakiuza miili yao huku wakijua
kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Washtakiwa
walikana na kurudishwa kutimiza masharti ya dhamana na shauri lao litaendelea
tena Januari 13 mwaka huu.
NIPASHE
Zaidi ya
wafanyakazi 150 wa Shirika la Usafirishaji Dar es salaam ‘UDA’ wamefukuzwa
kazi Desemba mwaka jana.
Msemaji wa
Shirika hilo George Maziku alisema wafanyakazi hao wamepunguzwa ikiwa ni moja
ya mikakati ya kuimarisha utendaji wa shirika hilo.
Alisema
hatua hiyo imechukuliwa baada ya Shirika kugundua kwamba limeajiri wafanyakazi
wengi ambao hawana kazi za kufanya.
“Ni kweli
Shirika limeamua kupunguza wafanyakazi tangu Disemba30 mwaka jana,lengo ni
kuimarisha utendaji kazi na kuongeza ufanisi wa kazi”alisema Maziku.
NIPASHE.
Wizara ya
fedha imesema hatua za awali zilizoanza kuchukuliwa na Rais Jakaya Kikwete
kushughulikia maazimio ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji wa fedha zaidi ya
bilioni 300 za akaunti ya Tegeta Escrow zimewezesha wahisani kuanza kutoa
misaada waliyokua wameisitisha awali.
Naibu Waziri
wa Wizara hiyo Mwigulu Nchemba alisema katika nusu ya mwaka wa
kalenda wa fedha kulikua na changamoto nyingi ikiwemo wahisani kusitisha
misaada yao kwa Tanzania kusubiri maamuzi yaliyotolewa na Bunge kuhusiana na
sakata la Tegeta Escrow.
“Kama Taifa
tuanze misingi ya kujitegemea,tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo
halafu unategemea fedha za wahisani ni tatizo,”alisema Nchemba.
Alisema
kutegemea wahisani ni tatizo ambalo nchi inabidi kujipanga kuondokana nalo
kwani hali hiyo inakwamisha miradi kuchelewa kutekelezwa wahisani wanaposhidwa
kuleta fedha kwa wakati.
NIPASHE.
Makabidhiano
ya miradi ya ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia,likiwemo bomba la
kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es salaam kati ya Mkandarasi wa
Shirika la Petrol Tanzania TPDC yanatarajia kufanyika Juni mwaka
huu,baada ya kukamilika kwa asilimua 100.
Mwenyekiti
wa Bodi ya TPDC Michael Mwanda na kaimu Meneja mkuu Mhandisi Kapuulya
Musomba,mradi huo ulianzishwa mwaka 2010 mpaka sasa umefikia asilimia 94.
Musomba
alisema mradi huo umegharimu dola za Marekani 1.225 ambazo ni zaidi ya
trilioni 1.8 ambazo ni za mkopo.
Alisema
benki ya Exim ya China imechangia asilimia 95 huku Serikali ya Tanzania
ikichangia asilimia tano kati ya fedha hizo.
NIPASHE.
Mahaka kuu
ya Tanzania imeiandikia barua Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na uvuvi kwa ajili
ya kurejesha mali ikiwemo meli ya Tawariq na zaidi ya bilioni mbili za tani
296.3 za samaki kwa raia wawili wa China.
Kwa mujibu
wa barua hiyo iliyosajiliwa na msajili wa mahakama Disemba 17 imeitaka Serikali
kurejea ahadi,kupitia hati ya kiapo iliyotolewa na Godfrey Nanyaro,Dk Charles
Nyanlundana na Katibu mkuu a Wizara hiyo.
Kwa mujibu
wa msajili huyo kiapo kinasema endapo washtakiwa hawatakutwa na hatia
mahakamani Serikali italipa gharama za samaki waliokutwa nao wa tani 296.3
ndani ya siku 30 tangu kuachiwa na mahakama.
Mbali na
barua hiyo mahakama kuu imeambatanisha nakala ya umri ya kuuza samaki hao
uliotolewa Desemba 11 na jaji Radhia Sheikh hukumu ya kuwaachia huru mahakama
ya rufani na hati ya mkurugenzi wa mashtaka nchini ya kuwafutia mashtaka.
MWANANCHI.
Shirikisho
la soka Tanzania TFF limepata nguvu kwani linatarajia kupata dola
milioni 1.3 sawa na bilioni 2.2 kutoka kwa Shirikisho la soka duniani FIFA
pamoja na fedha za kuiandaa timu ya Taifa ya Tanzania kushirikia mshindano ya
kombe la dunia mwaka 2018.
Katibu wa
FIFA Jerome Valcke alisema Shirikisho hilo limepanga kuwapa wanachama wake
bonasi ya bilioni 2.2 ikiwa ni sehemu ya mapato yake iliyoyapata baada ya kombe
la dunia la Brazil kumalizika mwaka jana.
Mbali na
fedha hizo pia FIFA itatoa milioni 10 kwa kila mwanachama katika kuziandaa timu
zao za Taifa kwa ajili ya kombe la dunia.
MWANANCHI.
Baadhi ya
wanawake wa Kitanzania waliofungwa katika magereza ya China na Hong Kong
walishika mimba kama moja ya mbinu za kutumia kupitisha dawa za kulevya bila
kugundulika kwenye uwanja wa ndege na mipaka mingine ya kimataifa.
Watanzania
wanne walioko katika Magereza ya China na Hong Kong walijifungua watoto kwa
nyakati tofauti wakiwa wanatumikia vifungo na wamekiri kuwa walibeba ujauzito
kama mbinu ya kuwasaidia kusafirisha dawa hizo bila kukaguliwa.
Watoto
wanaozaliwa magerezani baada ya kufikisha mwaka mmoja hupelekwa katika vituo
vya watoto yatima na kusomeshwa na Serikali ya China hadi pale wazazi wao
watakapomaliza kutumikia adhabu.
Imebainika
kuwa watoto wawili wapo katika vituo hivyo,mmoja tayari yupo Tanzania baada ya
kurudishwa na bibi yake na mwingine bado yupo gerezani na mama yake.
MWANANCHI.
Polisi
imewakamata vijana 510 wanaodaiwa kujihusisha na mtandao wa uhalifu maarufu
kama Panya Road katika Wilaya za Kinondoni,Ilala na Temeka.
Wazazi na
walezi wa watuhumiwa hao wameonywa kutokwenda kwenye vituo walivyohifadhiwa
vijana hao hadi polisi watakapojiridhisha na upelelezi.
Januari 2
maeneo mbalimbali ya Jiji yalikumbwa na taharuki kubwa kwa saa 2 baada ya
kuwepo na uvumi wa kuwepo kwa kundi hilo mitaani na kupora mali za watu.
Baada ya
tukio hilo Polisi waliendesha msako mkali na kuwakamata vijana 36 wenye rekodi
ya kufanya uhalifu.
Jana Kamanda
Kova alisema watuhumiwa wengine 510 walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya
vijiweni na wengine wakifuatwa katika nyumba wanazoishi baada ya polisi kupata
taarifa za kiintelijensia.
|
No comments:
Post a Comment