KUPOTEA NDEGE YA AIR ASIA:- Miili 40 yaopolewa Baharini. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Wednesday, December 31, 2014

demo-image

KUPOTEA NDEGE YA AIR ASIA:- Miili 40 yaopolewa Baharini.

.com/simgad/
6
Kufuatia kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At ,miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo na utafutaji unaendelea.

Miili hiyo ilionekana ikielelea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.Na taarifa kutoka serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika ndege iliyopotea.

Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa imebeba abiria mia moja na sitini na wawili ikitokea Surabaya nchini Indonesia kuelekea Singapore,ilipotea siku ya Jumapili Desemba 28,2014.

7

8

5

2
Utafutaji wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu,na eneo la utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha nchi kavu na baharini.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria ikielea majini.

Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini iliopolewa na meli ya kivita .

1
141230111001_airasia_prayers_solidarity_976x549_afp
Sala za kuwaombea waliokuwa wasafiri katika ndege hiyo zinaendelea.

Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia Fernandes aliingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi .

Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.

Habari Na:-BBC Swahili.
UNGANANASI KATIKA  FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *