AJALI ARUSHA:-Tazama Picha za Hiace ilivyoharibika vibaya wakati ikiua watu 12 ,Arusha October 29,2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, October 30, 2014

AJALI ARUSHA:-Tazama Picha za Hiace ilivyoharibika vibaya wakati ikiua watu 12 ,Arusha October 29,2014.


Watu 12  wamekufa papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa baada ya basi  dogo aina ya Toyota Hiace maarufu kama kipanya walikokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mafuta.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo jana October 29,2014,majira ya saa 10 katika  eneo  Makumira  wilayani  Arumeru.




Sabas, alisema  ajali  hiyo  ilitokea baada ya kipanya hicho aina ya Nissan T 519 DBV kilichokuwa kikitokea  jijini  Arusha  kwenda  Usa River kuhama upande na kugongana uso kwa uso na  lori hilo  lenye  namba  za  usajili  T582 ACR lililokuwa  likitoka  Moshi mkoani Kilimanjaro kwenda Arusha Sabas alisema majeruhi wa ajali  hiyo   wamepelekwa  Hospitali  ya   Wilaya  ya  Tengeru kwa matibabu.

Alisema  miili ya marehemu hao   imehifadhiwa Hospitali  ya mkoa  wa Arusha ya Mount  Meru kusubiri ndugu kuichukua kwa maziko.

Alisema baada ya ajali  hiyo kutokea  dereva  wa  lori  hilo alikimbia   na kwamba polisi wanaendelea  kumtafuta.



Mganga Mkuu wa Hospitali ya rufani ya Mount Meru, Dk. Josiah Mray, alithibitisha kwamba walipokea maiti za watu 12 waliokufa papo hapo katika eneo la ajali.Dk. Mray alisema kuwa walipokea majeruhi mmoja ambaye hali yake ni mbaya.

Kamanda  Sabas hakutaja majina ya marehemu hao kwa kuwa zoezi   la   kuwatambua pamoja na majeruhi hao lilikuwa linaendelea na kuahidi kutoa taarifa baada ya kukamilika.

Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad