SOMA / PICHA:-Mtalam wa Karate wa Kimataifa Sensei Rumadha Fundi (MTANZANIA) azidi kupanda Thamani ya Kimataifa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, June 25, 2014

SOMA / PICHA:-Mtalam wa Karate wa Kimataifa Sensei Rumadha Fundi (MTANZANIA) azidi kupanda Thamani ya Kimataifa.


Sensei Rumadha Fundi, katika "Japan Karate-Do Federation KATA SEMINAR " aliyofanyika Jumamosi 6/21/2014 katika University of St. Thomas, Houston, Texas chini ya Master Sensei  Masataka Muramatsu Dan 8 ( Hanshi), master Tatsuo Takegawa Dan 7 ( Kyoshi), kutoka Japan na washiriki kutoka Marekani, Mexico na bara la Ulaya chini ya uandalizi wa Sensei Ramon Veras Dan 6 wa Houston, Texas, USA.akiwa pamoja na Master Muramatsu.



Si Mwingine bali yule yule mtaalam wa michezi ya karate wa kimataifa Sensei Rumadha Fundi aka Sensei Romi,kutoka Uswahilini mwenye makao yake mjini Texas,Marekani, tarehe 21 Juni 2014 alikuwa miongoni mwa wataalam wa kimataifa walio teuliwa kushiriki seminar maalumu ya "Japan Karate-Do Federation KATA SEMINAR " iliyoendeshwa na wataalamu walimu mabingwa kutoka Okinawa,Japan. 

Semina hiyo ilifanyika katika  University of St. Thomas, Houston,Texas,nchini Marekani.

Sensei Rumadha Fundi ni mwafrika pekee aliyeteuliwa kushiriki katika seminar hiyo. mtaalam huyu Sensei Rumadha Fundi mwenye mkanda mweusi na 3 Dan,ambaye pia ni mtaalam wa ngazi ya juu wa mazoezi ya Yoga,inasemekana kuwa uenda akaongezewa dan nyingine kutoka kwa baraza la utawala la mchezo huo lenye makao makuu yake kule OKINAWA,JAPAN.


Sensei Rumadha Fundi, katika "Japan Karate-Do Federation KATA SEMINAR " akiwa na Sensei Muramatsu na Sensei Tatsuo Takegawa toka Japan.


Sensei Rumadha na Sensei Ernie Salinas.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad