LIGI KUU EPL 2013/2014:-Mechi mbili kumaliza Msimu-Manchester City,Liverpool na Chelsea Ubingwa upo Mikononi Mwao huku Arsenal na uhakika wa kucheza UEFA msimu Ujao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 04, 2014

LIGI KUU EPL 2013/2014:-Mechi mbili kumaliza Msimu-Manchester City,Liverpool na Chelsea Ubingwa upo Mikononi Mwao huku Arsenal na uhakika wa kucheza UEFA msimu Ujao.


Kaimu Meneja wa Manchester United Ryan Giggs amepata pigo la kwanza baada ya timu yake kupokea kichapo cha goli moja kutoka kwa Sunderland siku ya Jumamosi (Mei 03,2014).


Sebastian Larsson wa Sunderland ndiye aliyezima ndoto za ushindi za Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford baada ya kupachika goli zuri katika dakika ya 29 kipindi cha kwanza.

Kwa matokeo hayo Manchester United inaendelea kubaki nafasi ya saba na pointi 60 huku Sunderland wakijihakikishia kutoshuka daraja baada ya kujikusanyia point 35 huku wakiwa wamebakiza michezo miwili.

Mabingwa watarajiwa Ligi Kuu EPL 2013/2014 Mechi walizobakisha.

CHELSEA LIVERPOOL MAN CITY
Mei 4: Chelsea v Norwich
Mei 11: Cardiff v Chelsea

Mei 5: Palace v Liverpool
Mei 11: Liverpool v Newcastle

Mei 7: City v Aston Villa
Mei 11: Man City v W Ham


Manchester City, wakicheza Ugenini huko Goodison Park, walitoka nyuma kwa bao 1-0 na kuifunga Everton bao 3-2 na kutwaa Uongozi wa Ligi Kuu Uingereza kwa kuwakamata Liverpool kwa Pointi 80 na wao kuongoza kwa ubora wa Magoli huku Mechi zikibaki 2 Ligi kumalizika  msimu wake wa 2013/2014.

Kipigo hiki kimeondoa matumaini ya Everton kucheza UEFA League 2014/2015 na kuipa nafasi hiyo Arsenal.

Sat 3 May 2014 - Premier League 2013/2014.

    West Ham 2 - 0 Tottenham 

    Aston Villa 3 - 1 Hull 

    Man Utd 0 - 1 Sunderland 

    Newcastle 3 - 0 Cardiff 

    Stoke 4 - 1 Fulham 

    Swansea 0 - 1 Southampton 

    Everton 2 - 3 Man City


Position Team Played Goal Difference Points
1 Man City 36 59 80
2 Liverpool 36 50 80
3 Chelsea 36 43 78
4 Arsenal 36 24 73
5 Everton 37 20 69
6 Tottenham 37 1 66
7 Man Utd 36 19 60
8 Southampton 37 8 55
9 Newcastle 37 -15 49
10 Stoke 37 -8 47
11 Crystal Palace 36 -15 43
12 West Ham 37 -9 40
13 Swansea 37 -2 39
14 Aston Villa 36 -15 38
15 Hull 36 -11 37
16 West Brom 35 -12 36
17 Sunderland 36 -19 35
18 Norwich 36 -32 32
19 Fulham 37 -45 31
20 Cardiff 37 -41 30


 Jumapili 4 Mei 2014.

1530 Arsenal v West Brom

1800 Chelsea v Norwich

Jumatatu 5 Mei 2014

2200 Crystal Palace v Liverpool

Jumanne 6 Mei 2014

2145 Man United v Hull

Jumatano 7 Mei 2014

2145 Man City v Aston Villa

2145 Sunderland v West Brom

Mechi za Mwisho za Msimu:-Jumapili 11 Mei 2014[Mechi zote Saa 1100 Jioni, Saa za Bongo]

Cardiff v Chelsea

Fulham v Crystal Palace

Hull v Everton

Liverpool v Newcastle

Man City v West Ham

Norwich v Arsenal

Southampton v Man United

Sunderland v Swansea

Tottenham v Aston Villa

West Brom v Stoke


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad