HABARI/PICHA:- Kinana atoa somo kisiwani Pemba hasa juu ya swala la Muundo wa Serikali katika Mchakato wa Katiba Mpya’’. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 04, 2014

HABARI/PICHA:- Kinana atoa somo kisiwani Pemba hasa juu ya swala la Muundo wa Serikali katika Mchakato wa Katiba Mpya’’.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya Mei 03,2014, kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba…….’’Katika hobuba yake,Ndg. Kinana amewataka Wananchi wa Kisiwani humo kutohadaika na Wanasiasa wanapita kila mahali kwa lengo la kulipotosha Taifa,hasa juu ya swala la Muundo wa Serikali katika Mchakato wa Katiba Mpya’’.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya Mei 03,2014, kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiendelea kuzungumza kwa kutoa somo wakati wa mkutano huo.

Makamu Mwenyekiti UWT,Bi. Asha Bakari Makame akizungumza kwa msisitizo mkubwa na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar,Ndg. Shaka Hamdu Shaka akizungumza machache na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya Mei 03,2014,kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

Vijana wa CCM, Fatma Juma Ramadhan (kushoto) na Halima Juma Hajj wakighani mashairi mazuri ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (hayupo pichani).




Sehemu ya picha mbali mbali za wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba wakifuatilia Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya Mei 03,2014, kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.Picha zote na Othman Michuzi.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad