Wafanyakazi
wa Shirika la Msalaba Mwekundu waondoa maiti kwenye kaburi la pamoja mjini
Bangui.
|
Afisa wa juu
wa Umoja wa Mataifa anasema ghasia za kidini zinazoendelea katika Jamhuri ya
Afrika ya kati zinaonekana kuwa mbaya zaidi.
Katika
taarifa ya Jumatano(Februari 19,2014) kamishna
anayehusika na maswala ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navi
Pillay alisema ukiukwaji mwingi wa haki unaendelezwa na kundi la wanamgambo
wanaojiita anti-balaka ambao amesema kwamba wanalenga kwa maksudi waislam
katika mji mkuu Bangui.
Pillay
amesema wanamgambo hao wanauwa na kuwabaka waislam na kuharibu nyumba zao na
wana nia ya wazi ya kuwazuia waislam kurudi kwenye makazi yao.
No comments:
Post a Comment