Watu 7 wamefariki na wengine 8 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika eneo Zero Zero wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 08, 2013

Watu 7 wamefariki na wengine 8 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika eneo Zero Zero wilayani Ngara mkoani Kagera.

Basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 227 CLA lililokuwa likitoka wilayani Ngara mkoani Kagera  kwenda wilayani Kahama mkoani Shinyanga  likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana na Lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T 621 ATD lililokuwa limepakia matofali katika eneo linalofahamika kama Ziro Ziro yaliyopo makutano ya Barabara ya kutoka wilayani Ngara kuelekea Nyakahura na ile iendayo nchini Rwanda kupitia Benaco leo (Agosti 08,2013) mchana.





Basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace liliua Watu 7 papo hapo na  wengine 8 kujeruhiwa.





Muonekano wa Lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T 621 ATD lililokuwa limepakia matofali likiwa limeharibika vibaya baada ya Basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace.


Hili ndilo  eneo linalofahamika kama Ziro Ziro yaliyopo makutano ya Barabara ya kutoka wilayani Ngara kuelekea Nyakahura na ile iendayo nchini Rwanda kupitia Benaco ambapo ajali hiyo ilipotokea na kuuwa watu 7.


Hili ndilo  eneo linalofahamika kama Ziro Ziro yaliyopo makutano ya Barabara ya kutoka wilayani Ngara kuelekea Nyakahura na ile iendayo nchini Rwanda kupitia Benaco ambapo ajali hiyo ilipotokea na kuuwa watu 7.


Hili ndilo  eneo linalofahamika kama Ziro Ziro yaliyopo makutano ya Barabara ya kutoka wilayani Ngara kuelekea Nyakahura na ile iendayo nchini Rwanda kupitia Benaco ambapo ajali hiyo ilipotokea na kuuwa watu 7.
Watu 7 wamefariki na wengine 8 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika eneo linalofahamika kama Ziro Ziro yaliyopo makutano ya Barabara ya kutoka wilayani Ngara kuelekea Nyakahura na ile iendayo nchini Rwanda kupitia Benaco .

Jeshi la polisi wilayani Ngara limesema kuwa ajali hiyo iliyotokea leo(Agosti 08,2013)  mchana na kulihusisha basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 227 CLA lililokuwa likitoka wilayani Ngara mkoani Kagera  kwenda wilayani Kahama mkoani Shinyanga na Lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T 621 ATD lililokuwa limepakia matofali.

Taarifa kutoka jeshi la polisi imesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Hiace kwa kutokuwa mzoefu katika barabara ambaye alikuwa akiendesha gari kwa mwendo kasi  na kuingia katika makutano ya barabara hiyo, bila kutazama magari mengine hali iliyosababisha gari lake kugongwa na Lori hilo.

Majeruhi wanane wa ajali hiyo wamelazwa katika hospitali ya Murgwanza huku miili ya waliofariki ikiwa imehifadhiwa katika hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara mkoani Kagera.



Source:Radio Kwizera FM.

3 comments:

  1. dah,Mungu azilaze roho za maheremu hao mahali pema na walojeruhiwa wapate nafuu mapema

    ReplyDelete
  2. Mwenyezi Mungu azilaze Roho za Marehemu Mahala pema peponi.... Amen.

    ReplyDelete
  3. Ni ajali ambayo inaumiza kwani kimefariki kichanga na mama yake mzazi aliyetoka kujifungua,kweli inauma na kuna taarifa wamefika 9 sasa waliokufa

    ReplyDelete

Post Bottom Ad