![]() |
Mpaka sasa
mamlaka haijatoa kauli yoyote kuhusiana na hasara ya mali pamoja na chanzo cha
moto huo.
|
![]() |
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya imesema moto huo ulikuwa "mkubwa sana" na kwamba chanzo chake bado hakijafahamika ambapo msemaji wa polisi nchini Kenya, David Kimaiyo, akitaka kuwepo kwa utulivu. |
Baadhi ya
abiria na watu waliokuwa wakitarajia kusafiri
kwenda nje ya nchi, walikwama kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere baada ya ndege za kutokea Kenya kusimamisha huduma kutokana na
moto uliozuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Uwanja huo
uliopo Nairobi ambao hutumiwa na ndege nyingi za kimataifa kuunganisha safari
zake katika nchi mbalimbali, ulisimamisha kwa dharura safari za ndege zikiwamo
za Shirika la Ndege ya Kenya (KQ) kwa siku nzima ya jana.
Taarifa
zilisema ndege zote zilizokuwa zitue uwanja wa Jomo Kenyatta kwa siku ya jana
hazikuruhusiwa, na zile zilizokuwa tayari angani zilielekezwa kutua kwenye
viwanja vya ama Mombasa, Kenya au Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
uliopo mkoani Kilimanjaro, Tanzania.
Kwa mujibu
wa taarifa, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, ambapo taarifa zingine
zilisema kuwa moto huo ulianza kuwaka saa 11 alfajiri na kusababisha usumbufu
kwa abiria na wale waliokuwa na shughuli zao kwenye uwanja huo.
Hata hivyo,
vikosi vya Zimamoto na Uokoaji vilifanikiwa kuuzima.
Ilielezwa kuwa moto huo
ulianzia katika chumba cha Idara ya Uhamiaji kinachotumiwa na wasafiri
wanaowasili.
Tukio hilo
limemfanya Rais wa Kenya, Bw.Uhuru Kenyatta kufika uwanjani hapo kujionea hali
ilivyo akiwa ameambatana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw.Joseph Ole Lenku na
Waziri wa Usafirishaji na Miundombinu,Bw. Michael Kamau.
Kutokana na
kufungwa kwa uwanja huo, marubani wamekuwa wakielekezwa kutumia viwanja
vingine, ukiwamo Mombasa, Eldoret na Dar es Salaam (JNIA) na Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Entebbe, Uganda.
Maafisa wa
serikali wanasema sehemu ya paa la Kitengo Namba 1 cha Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta lilianguka kutokana na moto huo, na kuwapa tabu sana
wafanyakazi wa kikosi cha uokozi kupambana na moto huo ulioanza mapema asubuhi.
Moto huu
umetokea katika siku ambayo Kenya inakumbuka mwaka wa 15 tangu mashambulizi ya
mabomu kwenye ubalozi wa Marekani jijini Nairobi.
Mashambulizi
kama hayo yalifanyika pia siku na muda huo huo kwenye ubalozi wa Marekani
jijini Dar es Salaam, Tanzania, ambapo matukio hayo mawili yaligharimu maisha
ya watu 220.
No comments:
Post a Comment