Watoto wa tarafa ya Murusagamba wilayani Ngara mkoani Kagera wataka Mila Potofu ziondolewe. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 10, 2013

Watoto wa tarafa ya Murusagamba wilayani Ngara mkoani Kagera wataka Mila Potofu ziondolewe.


Watoto wakifatilia  Kongamano la watoto wa shule za msingi Tarafa ya Murusagamba lililoambatana na michezo lililoandaliwa na Shirika la Right to Play kwa kushirikiana na Kabanga Nikel na Halmashauri ya wilaya ya Ngara  kwa lengo la kuwajengea watoto uelewa wa haki zao na wajibu wao katika maisha yao ya kila siku.






Kutoka kushoto Afisa ufundi ,Richard Msekela ,Afisa Mahusiano wa Kabanga -Nikel Teophili Selestin na Afisa Michezo wilaya ya Ngara Saidi Salumu wakifatilia kinachoendela katika  Kongamano lililoandaliwa na Right to Play kwenye uwanja wa shule ya msingi Murusagamba kata ya Murusagamba wilayani Ngara mkoani Kagera kwa lengo la kuwajengea watoto uelewa wa haki zao na wajibu wao katika maisha yao ya kila siku.










Kutoka kulia ni Joramu Wimo ,Mratibu wa Shirika la Right to Play Tanzania Kabanga Project,Afisa ufundi ,Richard Msekela na Afisa Michezo wilaya ya Ngara Saidi Salumu wakifatilia kinachoendela katika  Kongamano kwenye mchezo wa Soka katika uwanja wa shule ya msingi Murusagamba ambapo wenyeji  Murusagamba waiibuka kidedea na kondoka na Zawadi ya Seti Moja ya Jezi.

Washindi katika Kongamano hilo katika mchezo wa Soka , Shule ya Msingi Murusagamba waliondoka na Zawadi ya Seti Moja ya Jezi.


Watoto wa tarafa ya Murusagamba wilayani Ngara mkoani Kagera  wametoa ombi kwa Serikali Pamoja na Mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kuondoa mila potofu ambazo zimekuwa zikileta madhara kwa watoto mbalimbali hapa nchini pamoja na kusimamia sheria zinazowalinda watoto.

Watoto hao wameyasema hayo wakati wa Kongamano la watoto wa shule za msingi Tarafa ya Murusagamba lililoambatana na michezo lililoandaliwa na Shirika la Right to Play kwa kushirikiana na Kabanga Nikel na Halmashauri ya wilaya ya Ngara  kwa lengo la kuwajengea watoto uelewa wa haki zao na wajibu wao katika maisha yao ya kila siku.

Watoto hao wameonyeshwa kukerwa na mila zenye kuleta madhara kwa watoto na kuitaka jamii kubadilika ili kuziondoa pamoja na  kuiomba serikali na halmashauri kutunga sheria ndogondogo ili wale wote watakaovunja haki za watoto waweze kuchukuliwa hatua.

Miongoni mwa mila hizo kandamizi kwa mtoto walizozitaja ni pamoja na ndoa za utotoni,ubaguzi  wa mtoto wa kike katika familia na kufanyiwa matendo maovu na jamii.

Aidha watoto hao wameomba kufanyika midahalo ya mara kwa mara itakayowakutanisha watoto na kuwasikiliza shida zao pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo katika maisha ya kila siku na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja.


Vilevile baadhi ya watoto ambao walikuwa wakishiriki katika kongamano hilo walionyesha kufurahishwa na mkusanyiko huo ambao Bw.Jorami Wimo yeye ni Mratibu wa Shirika la Right to Play Tanzania Kabanga –Project  amesema kongamano hilo litakuwa endelevu kwa Wilaya ya Ngara na kwamba watoto watakuwa wakipatiwa masuala yanayohusu Afya ,Usalama barabarani  pamoja na Elimu ili kuwasaidia kufikia malengo yao.

Katika Kongamano hilo liliambatana na Michezo ambapo katika mchezo wa pete(Netball) Mshindi wa Tatu walikutana Mukubu Shule ya Msingi dhidi ya Murugunga na Mukubu kuwafunga magoli 7-3 ambapo mfungaji bora aliibuka Valalia Mvukiye huku Fainali Murusagamba Shule ya Msingi wakiibuka kidedea kwa kuwafunga Muganza magoli 9-6 na kupewa zawadi ya Seti Moja ya Jezi na Mpira.


Mabingwa  Murusagamba S/M.
Kwa Upande wa mchezo wa Soka ,Mshindi wa tatu  aliibuka ni Ntanga Shule ya Msingi kwa kuwafunga Rwimbogo bao 3-2 kwa Maximiliani Marchades,Oscar Emanuel na Amin Jackson kuwapa ushindi wa magoli hayo Ntaga huku Magoli ya Rwimbogo yakifungwa na Filiminus Venace na Isaya Simeo.

Aidha mchezo wa Fainali wa Mashindano hayo ya Right to Play kwa shule za Msingi za tarafa ya Murusagamba,Shule ya Msingi Murusagamba waliibuka Mabingwa kwa kuwafumua Muganza bao 2-0 kwa goli za Jaston Mathayo na Dickson Pambano.

Washindi katika Kongamano hilo katika mchezo wa Soka , Shule ya Msingi Murusagamba waliondoka na Zawadi ya Seti Moja ya Jezi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad